Thursday, March 31, 2011

Mpenzi akiwa si wa maana na wewe si wa maana


HUENDA ukawa ni msemo mgumu kidogo, na huenda pia wengine wasiuelewe kwa haraka lakini ukiona mtu hana mwenzi wa maana ni dalili kwa kiasi kikubwa kwamba hata yeye si wa maana.

Wa maana kwa kawaida hufanya mambo baada ya kutafakari na kutafiti kwa kina.
Na ukiona mtu mara nyingi amekuwa ni mwenye kulalamikia wapenzi wake kwamba aaah nilikuwa na fulani, tukaachana kwa sababu alikuwa na tabia mbaya, baadaye nikawa na fulani naye ni wa hovyo, nikawa tena na fulani wa hovyo kabisa, sijui Mungu huyu kwanini ananifanyia hivi..... hii ni dalili mbaya na ni lazima uwe makini na mtu huyo.
Ni kwamba unakutana na mtu ambaye tayari alishazaa, labda ni tayari alishakuwa kwenye ndoa, labda tayari alishakuwa kwenye uhusiano na wanaume au wanawake wengi, ni lazima uwe makini sana kabla ya wewe kuamua kama uwe naye maisha au la.
Watu wengi wabaya mara zote huwa ni maarufu sana wa kulaumu wengine, badala ya ukweli kuwa wao ndio wafanyaji makosa, huwatupia lawama walioachana nao kuwa ndio tatizo. Inakuwaje kila siku wao tu ndio wawe wakosaji? Ni uongo wa hali ya juu.
Kwanini uwe makini na mtu ambaye tayari alishakuwa kwenye ndoa au kuishi na mwanamke au mwanaume pamoja au kuwa na wanaume wengi au wanawake wengi katika maisha yake kwa maana ya watatu na kuendelea? Ni kwamba kuachana si jambo rahisi, kwa maana hiyo ikiwa mtu alifikia maamuzi ya kuachana na watu hao, ni kwamba akili yake ina matatizo, ni mtu mwenye kuamini kuwa suruhu ya shida ya kuikimbia, badala ya kuitafutia tiba ili itoweke.
Kitaalam mtu yeyote ambaye alishawahi kuachana hasa kama waliishi kama mke na mume, ni lazima uwe makini sana kuangalia sababu walizoachania. Kama kwa mfano anasema aaah mwenzangu ndio alikuwa mbaya, alikuwa anakwenda kwa wanawake wengine, aaah alikuwa anakwenda kwa wanaume wengine, ni kweli inawezekana ni hulka ya mtu kuendekeza ngono, lakini swali la kujiuliza ni kwanini leo na wala sio jana?

Eeeh ni kwamba kwanini ni leo huyo mwenzi wake anafuata wengine? Wakati mwingine utakuta wengine wana nyodo, kama ni tendo la ndoa, kulipata hadi ubembeleze weee kama unaomba kibarua. Kazi tumbeleze, unarudi nyumbani nako, unaomba weee hadi watu wa chumba cha pili wanasikia leo kuna jamaa anabembeleza nanihiii.
Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa kadri ndoa inavyodumu, ndivyo idadi ya kufanya tendo inapungua, nyodo huongezeka, utasikia mtu anakwambia aaah bwana eeeh jana nimekupa na leo unataka tena kwani mimi ng�ombe....aaah hata ng�ombe huwa anapumzika. Wapo pia wanaume utawasikia wanaongea maneno mabaya kwa wake zao kwa mfano �aaaah achana na mimi bwana, nimechoka�
Sio sawa. Ni lazima kama wanandoa mjitahidi kuwa na lugha nzuri. Watu wengi wamekuwa maarufu wa kulalamika, lakini ukichunguza sana utaona mabaya mengi yanatokea kutokana na kauli au matendo yetu. Utakuta mtu kwa mfano hata kama labda anakubali mfanye tendo wengine wanatumia kama vile hasira �si umesema unataka, haya basi njoo, njoo nataka kuwahi, kama hutaki mi naondoka�. Huwezi kufurahia ndoa katika kauli za kipuuzi kama hizi. Ndoa inataka maneno matamu, eeeh si ndiyo ndugu yangu, sio maneno ya kimagumegume, maneno makavu kama dagaa!!! Hainogi. Unapozungumza na mwenzi wako ni lazima kuwe na tofauti na vile unavyozungumza na watoto au ndugu ama mzazi. Kwa mfano kama amelala na umemtengea maji, hutapaswi kumwita ukiwa mbali, bali unamsogolea na kumgusa �baba nanihii, maji tayari amka wahi kazini�.

Huenda hii kauli ikawa ni ngeni kwa baadhi ya wanawake, hawajui kuwatengea maji, wala mswaki, wala kuwasafishia viatu wala kuwatengea chakula waume zao. Mwanamke ukiwa hivi, jua unakosea. Katika maisha, hata kama si kila siku, lakini unapaswa kufanya kati ya haya, si mbaya pia mume kumfanyia mwenzi wake haya. Mapenzi ni deni, fanya ufanyiwe, mfanyie naye aone na siku moja afanye.
Kanuni ya mapenzi ni kwamba ikiwa umeguswa kichwa, unajisikia raha, ni kwamba hata ukimgusa kichwa pia ataona utamu. Tafakari kwa makini haya, chukua hatua. Msingi wa kuwa na maisha bora yenye furaha katika ndoa ni kuwa makini kwa kila unachofanya.
Kabla ya yote ni lazima uwe makini katika uchaguzi.Siri nyingine iliyo ya msingi sana ni kwamba usikubali kuwa mwepesi wa kufanya mapenzi. Watu wengi wanaokimbilia kufanya mapenzi, ndio wale ambao wanaishia kuachana na wapenzi wengi.

Kabla sijamaliza ni kwamba kuna baadhi ya wasomaji wameuliza je mwanamke mzuri zaidi anayefaa ni yupi? Inategemea, lakini tafiti nyingi zinaonyesha inakuwa nzuri zaidi kama mwanamke anakuwa na umbo la kuvutia, umbo namba nane yaani si mwembamba sana si mnene sana, ngozi halisia, wajuzi wa mambo na majambozi kiasi kwamba hata kama umegombana bado unaweza kufunika uso wake ulionuna na kanga mkaendeleaaa aaaaah, byeeeeeee

Monday, March 28, 2011

Unavyoweza kuitumia simu yako kulinogesha penzi lenu


Kuwasiliana kwa njia ya simu za mkononi ni moja kati ya njia bora za mawasiliano ya kuboresha uhusiano kwa wapenzi. Mwenzi wako anapokuwa mbali na wewe, kwa kutumia njia hii, unaweza kumsogeza karibu yako na kufurahia sana uwepo wake.

Unapompigia simu mpenzi wako hakikisha maneno yako yanakuwa laini, zungumza naye kwa unyenyekevu na kumtia hamasa ya kuzidi kuzungumza na wewe. Kadhalika unapomwandikia meseji, kaa chini na utunge, siyo unamwandikia ‘sema mtu wangu, uko shwari? Umeshakula?’ Hii ni meseji isiyo na hamasa yoyote ya kimahaba.

Unapaswa kumtumia sms za mapenzi, tungo za mahaba, maneno ya utani na vichekesho. Unaweza kumtumia meseji nyingi kadri uwezavyo kulingana na uwezo wako kifedha, ingawa mitandao mingi ya simu za mkononi siku hizi huwa na ofa maalum ya kutuma sms nyingi kwa gharama ndogo! Unaweza kujisajili kila siku kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano na mpenzi wako.

Pamoja na kwamba uwezo wako kifedha, muda na majukumu vinaweza kukufanya uamue idadi ya sms utakazomtumia mpenzi wako, lakini ni lazima umtumie angalau sms tano kwa siku.

Meseji hizo hutumwa kwa muda maalum, mathalani baada ya kuamka asubuhi unapaswa kumtumia ujumbe mzuri wa kumtakia asubuhi njema na mafanikio katika kazi zake za kutwa hiyo.

Mchana, mtakie mlo mwema na kazi njema, alasiri mtumie ujumbe wa kichekesho. Usiku, mtumie ujumbe wa kumpa pole kwa kazi, kisha malizia kwa kumtumia ujumbe mwanana wakati wa kulala.
Kama nilivyoeleza awali, unaweza kutuma meseji nyingi zaidi kulingana na uwezo wako na muda huku ukizingatia majukumu yako ya kazi.

Inawezekana mpenzi wako huko aliko ana kazi nyingi na ratiba zake zinambana sana, kama ndivyo unapaswa kuhakikisha humtumii meseji nyingi sana, kwani unaweza kumkera kwa milio ya simu kila wakati, muda ambao yeye hutumia kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuboresha maisha yenu ya baadaye.

Ni vyema kuangalia sana ratiba yake ya mchana, kwa suala la kumpigia simu na kumwandikia sms. Unaweza kumpigia simu angalau mara mbili kwa siku, baada ya hapo ukamwachia muda wa kufanya kazi, kwani si busara kumsumbua mwenzi wako anapokuwa ana majukumu kazini.

Hata sms zako, zisiwe nyingi sana kama nilivyoeleza awali. Usiku, ni muda mzuri sana kwako, kumfanya mwenzi wako awe karibu na wewe zaidi kimapenzi. Kwa kutumia simu mnaweza kuchati kwa muda mrefu mkitumia lugha laini za mapenzi, pia mnaweza hata kukutana faragha kwa kutumia simu zenu.

Mnaweza kufanya kila kitu kwa sauti laini zitakazoamsha hisia zenu na kujikuta kila mmoja akiwa anaridhika kwa kusikia tu, sauti ya mwenzi wake.tu kama inavyosomeka , kumekuwa na matatizo mengi katika matumizi ya simu kwa wapendanao. Tangu simu za mkononi ziingie, naweza kusema zimevunja ndoa zaidi ya milioni moja.

Sunday, March 27, 2011

Mpenzi wako amepoteza msisimko na wewe, nini cha kufanya?

SINA shaka kwa wiki mbili zilizopita wakati nazungumzia mada hii utakuwa umejifunza kitu kipya katika maisha yako ya kimapenzi. Inawezekana kabisa, ulikuwa unahisi mpenzi wako hana msisimko na wewe, lakini bado ulikuwa huna uhakika hasa!

Ni mada ambayo sina shaka itakuwa imekutoa mchanga na kukuingiza katika ulimwengu mpya wa fikra.
Rafiki zangu, kubwa zaidi ambalo mnatakiwa kufahamu ni kwamba, mpenzi wako si kwamba hakupendi, bali amepoteza ule msisimko wa kimapenzi na wewe. Si tatizo geni katika ulimwengu wa mapenzi.

Ni tatizo lililowaumiza wengi na wakati mwingine husambaratisha uhusiano wa wenzi mbalimbali kutokana na tatizo hili. Umewahi kujiuliza, mpenzi wako unampenda kwa moyo wako wote, lakini anafanya mambo yanayoonesha wazi kuwa hana msisimko tena na wewe, nini cha kufanya?
Utaachana naye au utaendelea naye kama kawaida? Hebu tuone kipengele kifuatacho...

SI SABABU YA KUMWACHA
Rafiki zangu, kuna tofauti kubwa kati ya usaliti na kupoteza msisimko. Aliyepoteza msisiko siyo kwamba amepoteza kwa hiyari yake, bali ni kwa bahati mbaya.

Yamkini hata yeye anatambua kuwa anaumwa, lakini hana jinsi, hawezi kusema, anajikuta anaishia kufanya vituko, si kwa kupenda mwenyewe bali kwa bahati mbaya. Cha kusikitisha zaidi ni kwamba, anapokea huwa anagundua baadaye, anaweza kulia sana kutokana na kitendo kile, akawa anazidi kujiumiza mwenyewe, lakini suluhusho akawa hana.

Wakati napokea simu na ujumbe mfupi wa maneno kutoka kwa wachangiaji wa mada hii wiki iliyopita, nilipata ujumbe kutoka kwa dada mmoja ambaye ni msomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambaye hakutaja jina lake.
Ujumbe wake ulisomeka hivi; “Ahsante sana kaka Shaluwa kwa mada yako, imenigusa sana kwakweli.

Nasubiri kwa hamu sana hiyo wiki ijayo niweze kujua tiba yake. Nimeishi katika utumwa kwa muda mrefu sasa.”
Msomaji huyo anaweza kuwawakilisha wengine wengi wenye tatizo kama lake.

ALIYEATHIRIKA AFANYEJE?
Nimeona ni vyema nianze kwa kuzungumza na waathirika wenyewe wa tatizo hili. Kama maelezo yote hapo juu yanakuhusu na unajijua una tatizo hilo, ni vizuri kuwa makini na kipengele hiki.

Kwanza kabisa, kubali tatizo lako, halafu amini kwamba mwenzi wako hana tatizo isipokuwa wewe. Ukishajiweka katika hali hii ni rahisi kubadilika. Kama unahisi huwezi kubadilika au ni vugumu kurudi katika hali yako ya kawaida, zungumza na mpenzi wako na umweleze kila kitu kuhusu tatizo lako.

Tumia nafasi hiyo pia kuomba msamaha kwa mpenzi wako juu ya yote ambayo umeyafanya kwake na unahisi yalikwenda kinyume. Kuwa mkweli kwa kiwango hicho, kutampa nafuu kubwa mpenzi wako ya kukuweka sawa, maana atajua ulikuwa hufanyi makusudi bali unaumwa!
Fanya jitihada za pekee kwa ajili ya kurudisha msisimko wa kimapenzi kwa mwenza wako. Simu, sms, waraka pepe ni kati ya njia zinazoweza kukurejeshea msisimmo uliokuwa umepotea.

Kuwa naye karibu, cheza naye michezo ya kimapenzi, pendelea kushikana mikono mnapokuwa mmetoka pamoja n.k, hizo ni njia nzuri zaidi za kukufanya uwe na msisimko kama zamani.

JINSI YA KUMTIBU MUATHIRIKA
Hapa sasa tunaangalia pale ambapo wewe umegundua mwenza wako ana tatizo hili. Yapo mambo ya kitaalam unayopaswa kufanya ili kuweka mambo sawa hatimaye mpenzi wako arudi kwenye hali yake ya zamani.
Unajua cha kufanya? Twende tukaone...

Jiachie kwake
Akili na hisia zako zitambue kuwa huyo ndiye mpenzi wako wa kweli, kama hisia zako zitasema hivyo kwa kumaanisha, basi bila ya shaka utajiachia kwake kisawa-sawa!
Kujiachia kwake, kutamfanya aone jinsi unavyompenda na kuthamini penzi lake. Hapo utampa sababu ya kuanza kubadilika taratibu.

Mpe uhuru
Usimbane, mfanye awe huru kwa kila kitu. Wewe ni wake, kwahiyo huna sababu ya kumuwekea mipaka katika maeneo fulani. Uhuru huo utazidi kumsogeza kwako na kumfanya aanze kupuuza na kusahau kabisa aliyokuwa anawaza au kukuambia awali.

Mfundishe kwa kauli njema
Katika mapenzi kuna kukosea, kumbuka kwamba huyu ana matatizo, kwahiyo wakati mwingine anaweza akafanya kosa kubwa sana ambalo litakuudhi lakini ukishatambua kwamba mpenzi wako anaumwa, ni rahisi zaidi kumfariji!
Tumia ulimi wako vyema kwa ajili ya kumwelekeza na siyo kumfokea au kumtukana.

Mweleze alivyo na thamani
Thamani yake kwako ni kitu ambacho kinamuumiza kichwa kila siku, yawezekana hata machozi yake husababishwa na jinsi asivyoamini kama yeye ni wa thamani wako.
Hapa ni chaguo lako, kufanya chochote ambacho kitamfanya ajione wa thamani kwako. Kumshirikisha katika mambo yako hata yale ya siri sana, kutamfanya aione thamani yako bila hata kumwambia!

Mtengenezee furaha
Usikubali kuyaona machozi yake hovyo, siku kuwa mpigania furaha yake. Kama kuna kitu ameudhika ni vyema kumtuliza haraka.
Inawezekana kabisa siku moja ukawa umemuudhi, fanya haraka sana kumuomba msamaha ili mambo yaende sawa. Hakikisha anakuwa na furaha muda wote.

Thamini chozi lake
Anapokuwa katika matatizo ya kiafya au kifamilia, kiasi cha kulazimika kumwaga machozi, unatakiwa kuyathamini na kuyafuta. Kuwa naye karibu, mfariji na kumfanya asijihisi yupo peke yake.
Asione kwamba tatizo ni lake mwenyewe, mfanye atambe na aone kabisa kwamba hayupo peke yake, nyuma yake yupo mtu anayempenda ambaye atamthamini siku zote. Hii itamsaidia kwa kiwango kikubwa sana kumaliza tatizo lake.

Sasa ibuka mshindi
Unapofanya kitu kizuri na kufanikiwa, lazima ushangilie maana tayari unakuwa mshindi. Hii ni nafasi yako ya kushangilia na kujiona mshindi kwa kurejesha msisimko wa mwenza wako.
Nina imani umebadilika na utaendelea kufurahia mapenzi na mwenza wako.

MASWALI 10 YA KUJIULIZA KWA WAPENZI.

Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutukutanisha tena kupitia safu hii nikiamini kwamba umzima bukheri wa afya na unaendelea nyema na majukumu yako ya kila siku.

Mpenzi msomaji wangu, binafsi kuna wakati huwa nakaa na kujiuliza maswali mbalimbali kuhusu uhusiano wangu, yapo maswali ambayo nayapatia majibu lakini mengine naishia kuyapotezea.

Naamini siko peke yake yangu na leo nimeona niwaandikie maswali 10 ambayo kama uko kwenye uhusiano unatakiwa kujiuliza. Kumbuka sitayajibu bali majibu unatakiwa kuyatoa mwenyewe kisha kuyafanyia kazi.

1. Unaufurahia uhusiano wako?
Hili ni swali la msingi kujiuliza. Ni vizuri ukajua kama unayo furaha katika uhusiano wako. Ukibaini kwamba hauko na furaha ujue kuna tatizo na uamuzi utakuwa si kuendelea kumng’ang’ania huyo uliyenaye bali unatakiwa kumuacha.

Kumbuka maisha yaliyotaliwa na huzuni hayawezi kuwa marefu, unaweza kujikuta unafupisha maisha yako kwasababu ya mapenzi tu. Kwa maana hiyo leo hii kaa na ujiulize kama unaufurahia uhusiano wako ama laa, isiwe bora liende tu.

2. Uko tayari kwa mtoto?
Hili si kwa walioolewa/walioa tu bali hata walio katika uhusiano wa kawaida.

Uko na mpenzi wako, kaa jiulize kama unadhani ni wakati muafaka kujiachia kwake ili upate mtoto kabla ya kuoana? Ukiwa makini suala la kupata mtoto haliwezi kutokea kama ajali ni ishu ya kuamua tu.

Kama uko ndani ya ndoa pia, ni kweli mtoto ni sehemu ya furaha katika maisha yenu lakini unadhani mmejipanga kwa kulea kwa muda huu? Usifanye mambo kibubusa, jiulize kisha jibu utakalolipata ulifanyie kazi.

3. Lipi la kujibadilisha?
Chukulia kwamba umepewa nguvu ya kujibadilisha vile ulivyo. Unadhani ni kitu gani ambacho unahisi kinamkwaza mpenzi wako au kinamboa lakini huwezi kukiacha?

Naamini kipo hivyo kama utakibaini ni vyema ukakifanyia kazi hata kabla hujapewa nguvu hiyo ya kujibadilisha kwani kuendelea kuwa hivyo ni kuliathiri penzi lako.

4. Kipi kinakufanya uhisi unapendwa?
Unahisi huyo uliyenaye anakupenda? Kama ndiyo ni lazima ukae na kujiuliza sababu za kukufanya uhisi hivyo.

Unadhani ni kutokana na mambo unayomfanyia, muonekano wako au tabia zako? Haiwezekani ikawa unahisi tu kwamba huyo uliyenaye anakupenda bila sababu za msingi.

Ukishabaini yale yanayokufanya uamini kwamba anakupenda basi tia chumvi, hakikisha hutoki kwenye mstari, mtadumu.

5. Kipi kinakuchukiza sana kwa mpenzi wako
Huenda vipo vitu vingi vinavyokuchukiza kwa mpenzi wako, hilo siyo tatizo kubwa kwani huo ndiyo udhaifu tunaousema kwamba kila mmoja anao.

Huwezi kumpata mpenzi ambaye atakufurahisha kwa kila kitu, ni lazima yatakuwepo mambo kadhaa ambayo huyafanya na huwa yanakuchukiza. Katika hayo angalia moja kubwa kuliko yote kisha uanze nalo katika kukabiliana nayo.

Naamini si ya kukufanya uachane naye ila ukiyajua itakuwa ni rahisi kuyazoea kwani inawezekana naye ni vigumu kuyaacha mara moja.

6. Umejifunza nini kwenye uhusiano wako wa zamani?
Huko nyuma ulikuwa una mpenzi mkaachana kutokana na sababu mbalimbali. Sasa umempata huyo uliye naye sasa, je, umejifunza nini kutoka kwenye uhusiano wako wa nyuma?

Je, unahisi kuna ambayo ulikuwa ukiyafanya yaliyosababisha wewe kutengena na mwenzako huyo? Je uko tayari kuyarudia?
Katika hili namaanisha kwamba, kutoka kwenye uhusiano wako wa nyuma kuna mambo unayoweza kujifunza yatakayokusaidia kuboresha penzi lako la sasa na hatimaye kuweza kudumu.

7. Yapi unayoyapenda kutoka kwa mpenzi?
Kuna uwezekano mpenzi wako anakufanyia mambo yanayokufanya udate, ni yapi hayo? Kama yapo usisite kumwambia mpenzi wako ili ajue na awe anakufanyia hivyo kila siku.

Unapenda anapokutoa ‘out’? Unapenda anapokutania au anapokufanyia mambo ya kiutundu na kiuchokozi mnapokuwa faragha? Hili ni swali muhimu kwakuwa yawezekana mwenzako anafanya kwa kuwa anajisikia kukufanyia lakini hajui ni furaha ya aina gani unayoipata.

8. Anakupenda?
Hili ni swali ambalo kila aliye katika uhusiano wa kimapenzi anajiuliza. Ni lazima kila mmoja kujiuliza swali hilo kutokana na ukweli kwamba mapenzi ya sasa yamejaa usanii wa hali ya juu.

Unaweza kukuta mtu anakufanyia mambo yanayokufanya uamini anakupenda kwa dhati kumbe hamna kitu. Ndiyo maana nikasema kwamba kila unapokaa jiulize anakupenda kweli au unatwanga maji kwenye kinu.

9. Ngono ina nafasi gani kwenu?
Ni hili na jambo linalosababisha mtafaruku kwa wapenzi wengi. Unakuta mmoja anapenda sana ngono lakini mwingine siyo kiivyo.

Wewe kama wewe jiulize kama kukutana na mpenzi wako faragha kuna umuhimu katika kuliboresha penzi lenu?

Unadhani unaweza kuishia kumwambia unampenda bila hata siku moja kumwambia unahisi kuwa naye faragha? Hilo jiulize mwenye kisha jibu utakalolipata ulifanyie kazi.

10. Penzi lenu lina maadui?
Unadhani kila mmoja anafurahia kuwaona jinsi mnavypendana au wapo ambao ni maadui  wanaotamani siku moja mtengane?

Huenda wapo na unawajua kabisa. Unadhani kwanini wanauchukia uhusiano wenu? Wanaona mnaringa au ni roho zao mbaya tu? Kwa vyovyote vile, kikubwa ni kuhakikisha huwapi nafasi.

Tuesday, March 22, 2011

Bora uwe mpweke, ni mateso kuwa na mpenzi asiyejua maana.........

Kila mtu angeyaheshimu mapenzi, angejua jinsi ya kulinda hisia za mwenzi wake. Angeelewa maana ya kupenda, asingekuwa na shaka pale anapopendwa. Angeishi ndani ya mwenzake, hivyo kuumizana kusingekuwepo, migogoro mikubwa na kuachana isingetokea.

Migogoro mingi inatokea kwa sababu wengi wameyageuza mapenzi kama mchezo (game), hawajui kuwa saikolojia inaonya vitendo vya kuucheza shere moyo wa mtu. Kumfanyia hivyo mtu mwenye hisia za ndani na za kweli katika kupenda unaweza kuua bila kukusudia.

Katika sehemu ya kwanza ya makala haya wiki iliyopita, nilieleza kuwa kama hujawa tayari kupenda, kunyenyekea na kuheshimu ni vizuri ukakaa pembeni kwa sababu unaruhusiwa kucheza game na mtu lakini ni kosa kubwa kucheza game na moyo wa mtu.

Hata hivyo, nilitaka kila mtu awe makini anapokuwa anaingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu. Anapaswa kujihakikishia upendo kutoka moyoni badala ya kujaribu. Wengi walioingia kwa mtindo wa kupima kina cha maji, walilia kwa kusaga meno.

Lipo tabaka ambalo linakuwa limejitosheleza kuwa mapenzi hamna lakini wanang’ang’ania, matokeo yake wanauguza jeraha la moyo kwa muda mrefu. Wengine wakajipa ugonjwa wa moyo. Ni vizuri kuwa makini mno ikiwa unahitaji kupata thamani halisi ya penzi.

Pigania kuhifadhi moyo wako. Uweke katika himaya salama. Usijidanganye kwa penzi lisilo na uelekeo. Lenye sura ya upande mmoja. Wewe unapenda, yeye anakuchora, presha inakupanda na kushuka mwenzako hana habari hata kidogo, tena ikiwezekana atakucheka kama katuni.

Kuna watu hawaoni umuhimu wa hili, mpenzi maana yake ni msiri wa maisha yako. Unapokuwa umelala fofofo hujitambui, ubavuni kwako yupo yeye. Anaweza kukufanya lolote wakati wewe unaogelea ndotoni. Mpende akupendaye, vinginevyo utakumbana na maumivu yafuatayo;

HATOKUSIKILIZA IPASAVYO
Mapenzi ni hisia. Ni rahisi kwako kujua kwamba uliyenaye anakupenda kwa dhati mnapokuwa mnazungumza. Je, anakusikiliza kiasi gani?

Mtu ambaye hana mapenzi na wewe, hata umwambie kwa lugha gani hawezi kukuelewa. Tena inawezekana ulizungumza naye jana kwa herufi kubwa, lakini leo jua limechomoza anarudia yale yale.

Inawezekana ulimuonya kuhusu tabia ambazo zinasababisha heshima yake ipotee. Hakatazwi kuwa na marafiki wa jinsia nyingine, lakini mazoea yake siyo mazuri kiasi kwamba wanaweza kutembea barabarani wameshikana viuno. Ikiwa unamueleza habadiliki, huyo hakupendi.
Hakusikilizi kwa sababu hana hisia na wewe.

ATAPENDA KUKUFANANISHA
Haamini kama wewe ni mwanamke au mwanaume mwenye mvuto kamili. Akiona wengine barabarani ni rahisi kushawishika. Atajiuliza hivi huyu na wangu vipi? Huyu anaonekana ni mzuri zaidi. Anajiuliza maswali hayo kwa sababu hajakukubali. Shtuka mapema.

Mwanasaikolojia Brandon King katika makala yake: “Be aware with ones heart!” anasema kuwa ni rahisi mtu kujidanganya kwamba aliyenaye siyo chaguo sahihi kwa sababu yupo naye lakini hiyo hutokea kwa mtu ambaye mapenzi yake si asimilia 100.

Anasema: “Vitu vya thamani yeye huvichukulia ni rahisi. Hajui kama mpenzi wake ni wa gharama kubwa. Mtu wa barabarani labda kwa sababu tu amevaa kapendeza, yeye ataanza kumfananisha na mwenzi wake nyumbani na ikiwezekana kumuona bora.

“Wengine hawana uvumilivu, kwahiyo wanaweza kujikuta wakimwaga sifa kwa watu wa pembeni. Wakiendelea huharibu kabisa kwa sababu hujikuta wakiwaeleza hata wapenzi wao, kitu ambacho taaluma ya saikolojia katika eneo la mapenzi inakataza.”

Brandon anaonya: “Ni kosa kubwa kumsifia mtu wa jinsia inayofanana na mwenzi wako mbele yake. Mfano unamwambia mwenzi wako wa kiume kwamba ‘yule kaka mzuri jamani’! Hata kama huna hisia za ndani ya moyo wako lakini haiwezi kumpa picha nzuri, atajiona hayupo salama kwamba unavutiwa na mwingine.

“Fikiria na wewe upande wako. Mwenzi wako anamuona mwanamke na yeye anammwagia sifa, ‘dah yule manzi mrembo, wewe ungekuwa mrembo kama yeye ningejidai sana’! Bila shaka utaumia sana, kwahiyo na yeye ndivyo anavyoweza kupata maumivu.”

Anashauri: “Kila mmoja aridhike kwa jinsi mwenzi wake alivyo. Haikusaidii kitu kumuona bora wa jirani kwani kuna wenzako wanajiuliza huyo wako watampataje? Mheshimu na mtukuze mbele za watu.

Ukijenga imani kwamba mpenzi wako ni bora kuliko wote duniani, itakuwa na moyo wako utakubali.”
Itaendelea wiki ijayo…

Saturday, March 19, 2011

Dondoo za kuzingatia unapomtumia mpenzi wako zawadi


Ni wiki nyingine tulivu kabisa tunakutana kupitia safu hii nikiamini kwamba kwa rehema zake Mwenyezi Mungu umzima bukheri wa afya.

Mpenzi msomaji wangu, wiki hii nataka kuzungumzia kitu ambacho wengi wetu tumekuwa tukikipuuza sana lakini kimethibitika kuwa na nafasi kubwa ya kuliboresha penzi la wawili waliotokea kupendana kwa dhati.

Nazungumzia ishu ya wapenzi kununuliana zawadi. Hapa sizungumzii zawadi ambazo wengi wetu tumekuwa tukinunuliana siku za Sikukuu kama vile Iddi, Krismasi, Valentine na nyinginezo bali namaanisha zawadi nje ya siku hizo.
Kumtumia mwenzi wako zawadi ni kati ya mambo ambayo humfanya afurahie uhusiano wake na wewe. Hata hivyo, hakuna zawadi za moja kwa moja ambazo ni rasmi kwa ajili ya wapenzi lakini ni vyema ukamtumia zawadi kulingana na mapenzi yake zaidi.
Kwa kuwa wewe unamfahamu zaidi mwenzi wako, unaweza kujua zawadi gani ni nzuri zaidi kwake au anayopendelea kuliko aina nyingine.
Wiki hii nimechambua aina kuu za zawadi ambazo ukimtumia mpenzi wako utamteka hisia zake na ataona unamjali.
Mavazi
Mavazi ni kati ya zawadi ambazo zitamfanya mpenzi wako azidi kukupenda na kuwa karibu zaidi na wewe.
Aina ya nguo ambazo unaweza kumtumia mpenzi wako ni zile ambazo unaamini atavutiwa nazo au zile ambazo zitampendeza na kumfanya aonekane nadhifu.Hata hivyo, zipo aina za mavazi ambazo zimependekezwa zaidi kwa ajili ya wenzi kutumiana wanapokuwa mbali na hata wanapokuwa karibu.

Kama wewe ni mwanamke unataka kumtumia mpenzi wako wa kiume, mavazi yafuatayo yanafaa zaidi. Saa nzuri ya mkononi, nguo za ndani, lakini lazima uzingatie rangi ya bluu, bluu bahari au nyeupe kimsingi zisiwe za rangi zinazoficha uchafu.

Zingine ni fulana za ndani ‘singlendi’, fulana, mkanda wa suruali, simu ya mkononi, vitambaa vya jasho n.k. Hakikisha katika zawadi hizo, unaambatanisha na manukato mazuri hasa yale ambayo unajua atayapenda.
Haishauriwi kumtumia suruali au shati kwa sababu inaweza kuwa kubwa au ndogo, hivyo kupunguza ladha ya zawadi hasa kama atakuwa ameipenda sana.

Zawadi za aina hiyo, unaweza kumpa mwenzi wako ofa ya kwenda kuchagua moja kwa moja dukani lakini kama unajua saizi yake na una uhakika akivaa atapendeza, ruksa kumnunulia vitu hivyo na tena utakapopatia saizi yake vizuri ataamini uko makini naye na unampenda kwa dhati.

Kama wewe ni mwanaume na unataka kumtumia mpenzi wako wa kike zawadi, lazima uwe makini sana! Mavazi yaliyopendekezwa hapa ni pamoja na batiki (gauni, blauzi na sketi, blauzi yenyewe n.k), hereni, bangili, mkufu, simu ya mkononi, saa ya mkononi, nguo za ndani (kulingana na mapendekezo yake, kwa jinsi umjuavyo), sidiria, viatu n.k.
Kama umesoma vizuri utaona mwanamke anaweza kununuliwa vitu vingi zaidi (hasa nguo) tofauti na mwanaume. Hii inatokana na aina za mavazi na saizi zao kukaririka kirahisi zaidi au kutokuwa na saizi ya moja kwa moja. Mathalan, batiki, sketi na blauzi na vinginevyo. Kama kawaida, mavazi haya, ambatanisha na manukato mazuri, hasa yale ambayo ndiyo anayopendelea mpenzi wako.
Maua pia ni kati ya zawadi zinazopendekezwa na wataalamu wa mambo ya mapenzi. Maua ni mazuri sana kwa mwezi aliye mbali, lakini ni vyema kuzingatia na umbali uliopo kati yenu, kwani maua huweza kusinyaa kabla ya kumfikia (hasa kama ukimtumia yale halisi, kwani ndiyo haswa mazuri).

Hata hivyo, zipo zawadi nyingine ambazo unaweza kumtumia mpenzi wako kwa kuangalia vitu anavyovipenda sana.
Hii ni njia pekee ya kuonesha ubunifu wako na jinsi unavyomjali hata akiwa mbali kwa kumtumia vitu ambavyo huwa anavipenda lakini alipo hawezi kuvipata!
Mathalan, mpenzi wako anapenda sana zabibu lakini amekwenda mkoa ambao vitu hivyo havipatikani kwa urahisi, hii ni nafasi yako kumtumia.
Mathalan unajua kabisa anapenda sana kusoma vitabu lakini sehemu aliyopo hawezi kupata, basi nunua majarida, magazeti na matoleo yote ambayo hajayapata kisha mtumie, hakika utakuwa umemfurahisha sana na kumfanya afurahi kupata vitu hivyo.
Kwa leo naomba niishie hapo, lengo ni kukufahamisha kwamba zawadi ni kitu muhimu sana katika kuliboresha penzi lenu. Kwanza mpenzi wako aamini kwamba unampenda lakini pia unamjali.

Friday, March 18, 2011

Uvumilivu, unyenyekevu sifa zinazowashinda wengi!


INANIPASA nimshukuru Muumba wangu kwa kuwa yeye ndiye mlinzi na kiongozi wa maisha yangu, naamini bila yeye mimi na wewe tusingekuwepo, hivyo basi tuna wajibu wa kumshukuru kila wakati.

Bila shaka utakuwa mzima wa siha njema na macho na akili yako vimejiandaa kupata darasa hili murua kwa ajili ya maisha yako ya kimapenzi.

Yap! Leo nazungumzia mambo muhimu sana kwa wapenzi ambayo yanawachanganya wengi; uvumilivu na unyenyekevu! Kwa hakika ni maneno mepesi kuyatamka, lakini yana maana pana sana katika ulimwengu wa mapenzi.
Labda niweke wazi jambo muhimu, katika mada hii nitazungumza zaidi na rafiki zangu ambao wapo kwenye ndoa. Nazungumzia unyenyekevu na uvumilivu katika ndoa bila kujali jinsia, je ni utumwa? Hapa kila mmoja atakuwa na jibu lake, lakini leo nataka kuwapa ukweli wa kitaalamu.
Kuna usemi usemao ukitaka kujua uhondo wa ngoma uingie ucheze, wengine pia husema ukitaka kujua utamu na uchungu wa ndoa basi uwe mwanandoa.
Semi hizi zina ukweli ndani yake, wewe ambaye hujaingia kwenye ndoa naamini si rahisi kujua shida ama starehe apatazo mume ama mke ndani ya ndoa, pengine kama utazijua ni kwa kuzisikia kwa wanandoa ambao wanaeleza maisha yao.

Hata kama utayasikia hutajua ukweli yampatayo mwenzio mpaka yakukute mwenyewe kwani mengi huwa ya siri za ndoa. Kuna matatizo mengi wapatayo wanandoa, ukiniambia nitaje matatizo yaliyopo katika ndoa za watu  nitaeleza mengi sana kutokana na uzoefu wangu pamoja na tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalamu wa mambo ya mapenzi.
Lakini wakati nikizitaja kero za ndoa pia kuna upande wa pili ambao ni furaha, kuna mengi mazuri wayapatayo wanandoa wanapokuwa katika ndoa zao.

NDOA NI NINI HASA?
Ndoa ina maana kubwa sana katika maisha ya binadamu, hata hivyo ina tafsiri nyingi kulingana na imani au mahali ndoa ilipofungwa! Kwa Wanasaikolojia wa Mapenzi ndoa ni ukamilifu wa makubaliano ya muungano wa mwanamke na mwanaume wenye kupendana kwa lengo la  kuishi pamoja kama mume na mke kulingana na sheria ya  dini,  mila au desturi za sehemu fulani wakiwa chini ya sheria ya nchi.

Pamoja na tafsiri hiyo ambayo hutambuliwa na wataalamu wa mambo ya mapenzi, hawashauri wanandoa kuachana, maana kama waliungana kwa upendo basi wanapaswa kuishi kwa upendo na kusikilizana siku zote, huo ndiyo upendo wa kweli ambao Wanasaikolojia wa Mapenzi wanautambua.

NDOA INALINDWAJE?
Hapa ndipo kwenye msingi wa mada yetu, unapoingia kwenye ndoa kitu cha kwanza unatakiwa kufikiria jinsi ya kuilinda ndoa hiyo kwa gharama yoyote! Kuingia kwenye ndoa na kutoka baada ya muda mfupi ni kujitafutia laana ambayo haina ulazima wowote.

Hapa unatakiwa kufikiria mpaka mwisho wa uwezo wako wa kufikiri ili ndoa yako idumu na usije ukajikuta umeingia katika laana hiyo. Linapokuja suala la ulinzi wa ndoa yako, utashindwa kumnyenyekea mpenzi wako?

Unatashindwa kumvumilia mpenzi wako kwa sababu utajihisi wewe ni mtumwa wa mapenzi? Wapi imeandikwa hii? Mathalan mkeo anaumwa na kwa bahati mbaya hamna msichana wa kazi, je utashindwa kumsaidia kazi kama kupika, kufua, kuosha vyombo na kazi nyinginezo kwa sababu tu, wewe ni mwananume? Haingii akilini hata kidogo.

Rafiki zangu, hii ni mada ambayo inahitaji umakini wa kutosha kuweza kuelewa ninachokizungumzia. Ninaposema uvumilivu namaanisha nini hasa? Twende tukaone hapa chini.

UVUMILIVU
Katika maisha anayohitaji kuyavumilia mwanadamu ni maisha ya ndoa. Ndoa inakuwa na mambo mengi sana, kutunza familia, kupeana haki za nyumba, kusaidiana na kuvumiliana katika vipindi vya dhiki na faraja na mengineyo.

Ukarimu, uaminifu, upendo wa kweli ni kati ya chachu za kudumisha penzi na kamwe halitaweza kuchuja. Unapooa au kuolewa lazima ufahamu kuwa unakuwa umejenga undugu baina ya familia yako na ya mwenzio.
Katika kuishi kwenu huko utakutana na matabaka mengi, watu hutofautiana tabia, mfano wewe mwanamke umeolewa, mumeo akaleta ndugu, yaani wifi zako. Unatakiwa kuwasoma wifi zako tabia ili uweze kuendana nao.

Katika hili, ili uweze kufanikiwa unapaswa uwe na busara, mvumilivu, mnyenyekevu, na kuonesha kuwajali, hii inaweza kukusaidia sana kwani watakapokutendea mambo ya ajabu nawe ukaanza kuwaropokea matusi, utakuwa unajingiza kwenye migogoro ambayo mwisho wake huweza kuwa mbaya zaidi kwako kuliko kwao.

Kumbuka kuwa Mungu ametuumba kila mtu na udhaifu wake, ndiyo maana unaona wanandoa wengi wanajikuta wakizikimbia ndoa zao kwa kutendwa na wandani ama ndugu wa wandani wao, wakati mwingine mume anaweza kuwa hajui, unayepaswa kumweleza ni wewe.

Wakati unamweleza lazima uzingatie heshima na busara ambayo haitaonesha kwamba umedharau ukoo wao. Siyo unaanza kusema: “Nyoo! Umeniletea ukoo wenu hapa, chakula hakitoshi! Nitawafukuza!”

Kwa kauli hiyo utaonekana limbukeni, kaa naye chini zungumza naye kwa ukarimu mweleze ni jambo gani  linalokunyima uhuru wewe kama mkewe wa ndoa. Usimfiche, mwambie kwa upendo: “Mume wangu, kuna jambo wifi amenitendea sijui kama anaona ni kosa lakini miye naona amenikosea, mweleze asirudie tena.”

Kauli hiyo hapo juu ni tiba tosha kwa mumeo. Tena hakikisha wakati unamweleza haya mpo peke yenu chumbani na huenda ni baada ya kumpa haki yake. Ni kauli nzuri ambayo itamjenga na kwa hakika atalifanyia kazi jambo hilo.

Huo ndiyo uvumilivu ninaouzungumzia, siku zote wewe ndiye unayetakiwa kuwa na uchungu na ndoa yako. Kabla ya kuzungumza jambo lolote fikiria mara mbili, halitasababisha matatizo kwako? Ukipata matatizo au kuachika huyo wifi yako atakuwepo? Jibu ni hapana! Utakaporudishwa kwenu, utawaangaliaje wazazi wako ambao walikulea katika malezi mazuri na kukufunda vyema? Ni nini kama siyo aibu mtoto wa kike utakuwa umewapelekea wazee wako?

Kaa chini, fikiria kwa makini kabla ya kuamua jambo lolote linalohusu ndoa yako. Kumbuka kuwa kuingia kwenye ndoa ni kazi ngumu lakini kazi ngumu zaidi ni kuhakikisha unailinda ndoa hiyo iendelee kuwa hai siku zote.

Hapana shaka siku mnasherehekea miaka 10 au jubilee ya ndoa yenu, utakuwa ukijimiminia sifa kwamba kama siyo uvumilivu wako usingeweza kufikia hatua hiyo. Rafiki zangu, napenda sana kuendelea lakini nafasi yangu haitoshi, hadi wiki ijayo tena katika sehemu ya mwisho ya mada hii. USIKOSE!

Monday, March 14, 2011

Nidhamu ya kweli kwenye mapenzi ni tulizo la moyo, uhuru-2


Omba Mungu kila siku akupe maisha yenye dira. Akujalie hekima za kuijadili hasi kabla ya kuiacha ipite. Vivyo hivyo kuitafakari chanya kwa kiwango kinachotosha. Soma kwa mtindo wa katikati ya mstari upate kunielewa.
Mungu ameniwezesha kuanza sehemu ya pili ya makala haya kwa mtindo huo. Ninaposema jadili hasi nakuwa namaanisha kuwa si kila unayemuona mbaya, anaweza kuwa hivyo daima. Kuna leo na kesho!

Inawezekana ulidanganyika kuwa ni mbaya. Usifanye vituko kwanza. Onesha ustaarabu, jiweke katika mazingira ya mtu mwenye hekima zake, acha kichwa kiwe kitupu ili baadaye ufanye uamuzi sahihi baada ya kujiridhisha kwa alama za kila upande.

Tafakari chanya! Hoja kuu ni kwamba aliye mbele yako usidhani ni mwema kabla ya kumchambua. Kuna waliohadaika kwa uzuri wa ukakasi kumbe ndani yake kuna kipande mti. Ukaona anang’aa kumbe yeboyebo. Tobaa!

Siku zote, unatakiwa uishi katika misingi ya adabu! Usithubutu kufanya yasiyofaa kwa kigezo cha kudhani mwenzi wako upo naye kwa kuzugia. Kesho mnaweza kuwa mume na mke, halafu ukakumbushwa uliyofanya ukajisikia vibaya.

Hapa naelekeza nidhamu ya kweli katika mapenzi ili uwe huru daima. Unatakiwa ujiweke salama wakati wote. Usiruhusu maovu yako yajulikane kwa mwenzi wako, kwani mwisho wake ni mbaya.

Ulikuwa mtu wa ‘totoz’, hizo ni ‘faulo’ za zamani, lakini hupaswi kuona ni ufahari, ukasimulia hovyo. Ipo siku utathubutu kumsimulia mkweo, matokeo yake siku unapeleka posa akakutoa mbio.

Ulikuwa mtu wa kuchuna mabuzi, usiku viwanja, ukawa unaruka ‘fensi’ nyumbani kwenu kwenda kulala hotelini, unadhani hiyo ina faida gani kumueleza mwanaume uliyeanza naye uhusiano juzi? Kuficha kucha ni nidhamu ya kimapenzi.

Unatakiwa ujitunze kuanzia mdomoni mpaka matendo hasa unapokuwa na mtu wako. Msome kabla ya kuanza kuzungumza historia ya maisha yako. Lakini kubwa ni wewe mwenyewe kujiuliza kama hilo unalotaka kumwambia lina manufaa yoyote.

Mathalan, mtu wako wa zamani alikuumiza, kwahiyo hakuna ubaya wowote ukimueleza kwa maana ili ajue linalokusumbua na afahamu jukumu lake la kukupa faraja. Ni kosa kumwambia jinsi unavyomkubali.
“Nimeachana naye lakini namkubali sana.” Hii ni kauli ambayo haipaswi kutolewa na mtu mwenye mawazo chanya katika mapenzi. Wakati unaongea hivyo, ni vizuri ukajua kuwa naye neno hilo akilisema kuhusu mtu wake aliyepita litakuchoma, utaumia.

Unashauriwa kisaikolojia kusema mabaya ya mwenzako aliyepita mbele ya mtu wako wa sasa. Hata hivyo, hutakiwi kufanya wimbo kwa maana kwa mwenye uelewa atajua bado unakumbuka penzi lake. Chuja ya kuzungumza.
Pointi hii inatoa mantiki kwamba katika maisha yako, hakikisha yanayomhusu mtu wako wa zamani unayajadili na wengine kama unaona inafaa, Si kuyaweka mezani kwa mpenzi wa sasa. Wengine wana nongwa, atakukumbusha kila siku mpaka utaona kero.

TOA KIPAUMBELEA KWA MWENZI WAKO
Ni kosa kubwa kumuweka mwenzi wako kwenye mzani. Katika hilo unashauriwa kumfanya namba moja kila siku. Wiki iliyopita nilieleza ‘ushpesho’ alionao kwako, kwahiyo ukimdharau aibu iwe kwako.
Tafakari kwamba baada ya kumaliza shughuli za kila siku, wewe na yeye mnalazimika kuwa chumba kimoja, mnalala kitanda kimoja na ikiwezekana mnawekwa kwa ukaribu na shuka moja. Unaamka asubuhi huna kovu, upo salama kabisa.

Mwenzi wako ni mlinzi namba moja wa maisha yako, kwahiyo unatakiwa kumjali wa kwanza kabla ya yeyote yule. Rafiki akisema nawe ukazingatia na kupuuza alichokitamka mwenzako ni kosa kubwa. Fanya mapitio ya tabia yako leo.

Ushauri kuhusu nidhamu yako katika mapenzi, inakutaka uachane na mawazo yenye kuganda. Kwa hali yoyote ile, unatakiwa kumkubali alivyo na umpe thamani inayostahili. Usihadaike na macho, dunia ni ya wawili kwa maana wewe na yeye!

POTEZA KUMBUKUMBU ZA KUUDHI

Iwe ulikosea mwanzoni au kwa namna yoyote ile, fanya juu chini uweze kupoteza kumbukumbu ambazo zinaweza kumuudhi mwenzi wako. Hili ni la lazima kwako ikiwa unataka kusimamia nidhamu ya kweli kwenye mapenzi.
Itaendelea wiki ijayo…by nico trac 0716 276 000

Faida na hasara za wapenzi kutambulisha uhusiano wao.

Watu wengi hupenda kuwa na uhusiano wa kimapenzi ulio wazi mbele ya jamii. Kitaalamu hili ni jambo jema, lakini linahitaji umakini katika kulitekeleza.

Wapenzi wengi nyakati hizi wamekuwa wepesi mno kuiweka wazi jamii juu ya uhusiano wao bila kujali faida na hasara zake. Ni rahisi kukutana na watu wa jinsia mbili na kupata utambulisho huu: “Huyu ni mpenzi wangu, mchumba wagu naomba, umsalimie.”

Tafiti za masuala ya mapenzi zinaonesha kuwa miongoni mwa mambo yanayowafurahisha wanawake wengi nyakati hizi ni utambulisho. Dk. Robin Baker mshauri na mwanasaikolojia nchini Uingereza anathibitisha hili kwenye uchunguzi wake.

“Kwa nini hujanipeleka kwenu? Mbona hutoki na mimi kwenye mapumziko yako na rafiki zako mwishoni mwa wiki? Jamani napenda twende wote klabu.” Hizi ni kauli za kiu ya utambulisho wa uhusiano kwenye jamii.

Nikiweka sawa mwenendo wa mada hii, nisiwatenge wanaume kwa mbali, kwani nao hutajwa kuwa ni hodari wa kutangaza uhusiano wao na wasichana hasa warembo au wenye nafasi fulani kwenye jamii, lengo likiwa ni kujisifu na kuuambia umma kuwa “mmiliki wa mali ni mimi.”

Kama nilivyotangulia kusema, hilo ni jambo jema, lakini swali linabaki kwenye swali nani ajuaye faida na hasara za uhusiano ulio wazi kwenye maisha ya mapenzi? Bila shaka akili yako msomaji inatafuta majibu!

Rejeo la Utafiti wa Taifa la Waingereza linaonyesha kuwa wanawake wanane kati ya kumi na wanaume sita kati ya kumi walikiri kuwa udanganyifu kwenye uhusiano wao wa kimapenzi.

Hoja inayozaliwa kwenye utafiti huo ni hii: “Kuna faida gani kumtambulisha mpenzi mdanganyifu kwenye jamii?” Labda kabla ya kwenda huko tupitie faida za uhusiano wa wazi ambazo ni:Kujenga uaminifu, kuthibitisha chaguo, kufungua ukurasa wa kujisahihisha, kujifunga kwenye ramani ya penzi la kweli.

Baada ya kutazama faida tusonge hatua moja mbele kutazama hasara ambazo nyingi zimeanishwa na Dk. Robin kuwa ni za kisaikolojia. Inaelezwa kutambulisha penzi la mdanganyifu ni sawa na kupanda mti wa uchungu pale penzi litakapovunjika.

Ifahamike kuwa kadiri idadi ya wanaofahamu uhusiano inapokuwa kubwa ndivyo maumivu ya kuachana yatakavyokuwa. Jaribu kufikiria mtu ambaye umemtambulisha kwa wazazi, ndugu na marafiki halafu anakusaliti utawaambiaje uliowajulisha?

Ni wazi litakuwa jambo gumu kuwaambia wote, hii ina maana utakuwa utajiona mnyonge kila siku, wakati mwingine si kwa ajili ya kusalitiwa kwako bali kwa sababu rafiki yako amekutumia meseji ya kukuuliza hali ya mwenzako.

Nashauri wapenzi wasitambulishane haraka haraka bila kuchunguzana vinginevyo wakisalitiwa watapata ugonjwa wa moyo. Ni nafuu kuachana na mwanaume asiyejulikana kwa marafiki zako, kuliko uliyemtambulisha kwa mbwembwe kwa ndugu zako na kuonekana naye mtaani kila siku.

Si kila mtu ni mshauri mzuri katika maisha.

KUMEKUWA na tabia za watu kuingilia matatizo ya watu wakionyesha kutaka kutoa msaada ambao huwa kinyume chake.

Badala ya kutengeneza wanaharibu kabisa. Inakuwaje umekosana na mwenzako pengine kosa lenyewe lipo katika maisha yetu ya kila siku, kwa vile si wote tuliokamilika, lakini watu walishikie kidedea.
Kwa hali hiyo tatizo lolote ndani ya nyumba zetu kwa kulitoa nje laweza kuwa silaha ya kuwaangamiza.

Si wote waliofurahia utulivu wenu, wapo watakaokuvunja moyo kwa kuongeza maneno yao ambayo kwa mtazamo wako wa haraka utaamini kabisa watu wale ni wema lakini mwisho wa siku unagundua ulifanya maamuzi kwa faida yao.

Nasema hivi kwa nini?
Nina mfano hai katika tukio moja siku za nyuma lililotokea Marekani la mwanamuziki Chris Brown kumpiga mpenzi wake Rihanna, jambo lile ni la kawaida kwa wapenzi kukosana hata kufikia kupigana.
Lakini jambo lile lilipofika mbele za watu kuna watu walitaka kujenga umaarufu kupitia tatizo lile. Walilisimamia kidete na mwisho wa siku wawili wale walitengana.

Simamini kama Rihanna baada ya kupigwa na mpenzi wake uamuzi wake ulikuwa kuachana na Brown, pengine baada ya tukio lile hasira zilitawala lakini kama angekaa chini angeweza kutuliza hasira zake na kumsamehe mpenzi wake. Lakini shinikizo la kila mtu ndilo lililomfanya Rihanna kuamua kuachana na Brown.

Sikutaka kisa hiki kiwe mada ya leo, bali nilitaka kutoa mifano hai ambayo huvunja penzi la wawili hata kama mnapendana. Mara nyingi panapotokea tatizo ndani ya uhusiano si wote washauri wazuri ndiyo maana kuna siku nilielezea sababu za mtu kutousemea moyo wa mtu.

Katika uhusiano kuna kitu Uvumilivu:
Huu ndiyo uliobeba mambo mengi katika uhusiano na hadi leo kuna watu wameishi muda marefu katika ndoa zao. Si kwamba katika maisha yao waliishi kama malaika, bali walivumiliana.

Haohao kuna kipindi mazungumzo yao ya ndani yalishindikana lakini wazazi au watu wenye busara walipowakalisha chini waliwasikiliza na kumaliza tofauti zao.

Siamini waliomshauri Rihanna aachane na Brown katika uhusiano wao hakuna migongano, wanaishi kama malaika wasiotendeana makosa. Tumeshauriwa tutenganishe ndoa za watu zilizokosa suluhu ya kuwa kwao pamoja kuna hatari siku za mbele. Lakini tatizo la kawaida ni kupatanisha, hata vitabu vya dini vimemsifu mpatanishaji na si mvunjaji.

Lakini matatizo ya Brown na Rihanna ni ya kawaida si ya watu kuyabebea bango ili kuwatenganisha wawili hao. Nimekuwa nikiendelea kutumia mfano huu baada ya kuona baadhi ya watu wamekuwa wakifurahia kutengana kwa watu na si kuwaunganisha.

Hii imekuwa hasa katika jamii yetu mtu akikueleza tatizo lake badala ya kumpa ushauri wa kujenga wewe unabomoa kabisa.

Nataka nizungumze kitu kimoja, katika maisha yetu kukosana ni sehemu ya maisha ya mwanadamu, kiumbe mwenye mapungufu. Kama mnapokosana kitu cha kwanza itafute suluhu ndani kwa kuzungumza na mwenzako, pengine alifanya kwa hasira lakini ikitulia uweza kugundua kosa lake.

Pili kama ndani itashindikana basi tumieni wazazi wa pande mbili au watu wazima wenye busara. Na hapo ikishindikana mnaweza kwenda mbele zaidi hata katika mabaraza ya usuluhishi, lakini kwa watu waliokubali mioyoni mwao kuwa kitu kimoja kuvumiliana kwa shida na raha kwa uzima na ugonjwa ni wepesi kurudi katika ubinadamu na kumaliza tatizo lao.

Namalizia kwa kusema, linapotokea kosa lolote usikurupuke kwanza kulipeleka mbele za watu, lipime ni bahati mbaya au makusudi je, wewe upo sahihi kila siku. Ukipata jibu ni rahisi kumsamehe mwenzako.

Jiepushe kulitoa mbele za watu kila tatizo lako la ndani, pia usikubali kila ushauri. Upime kwanza kabla ya kuupokea na kuufanyia kazi.

Monday, March 7, 2011

UTAJUAJE KAMA WEWE NI MTUMWA WA MAPENZI!

Hii ina maana pana sana, lakini naweza kutoa moja kama mjumuisho wa yote! Utumwa wa mapenzi unaweza kutokea pale, utakapompenda mtu ambaye hana habari na wewe kabisa, yaani unajikuta ukioza juu yake, lakini anakuwa hana mapenzi na wewe kabisa.
Wakati mwingine unaweza ukamshawishi mtu huyo kwa vitu fulani, akakubali kuwa na wewe lakini sio kwa mapenzi ila kwa kuwa kuna kitu fulani atapata kutoka kwako.
Kama ukiruhusu utumwa wa mapenzi, maisha yako ya kawaida, yanaweza kuharibika na kukosa muelekeo! Uwezo wako wa kufikiria utakuwa mdogo ma hata wakati mwingine kupunguza ufanisi wako wa kazi.
Muda mwingi utautumia kufikiri kwanini fulani hakuipendi? Una kasoro gani n.k, kimsingi kama ukiruhusu utumwa wa mapenzi, mpangilio wa maisha yako unaweza kuharika na kukosa muelekeo kabisa.

UTAJUAJE KAMA WEWE NI MTUMWA?

Hili ni rahisi kutambua ingawa ni hatua mbaya sana katika maisha yako. Jambo la kwanza ni mabadiliko ya hisia za moyo wako, utajikuta ukimpenda mtu sana, ambaye hata time kabisa na wewe! Pamoja na kuwa anaonyesha kila dalili za kukuchukia lakini bado utahisi kumpenda na kumhitaji katika maisha yako.
Moyo wako huendele kuysisitiza kuwa huyo sio sahihi kwa maisha yako, lakini bado mtu huyo ataendelea kukuonyesha kila vibwanga vya kuchukiza. Sio jamboi la ajabu kuhiusi kufa kuliko kuendelea kuteseka kwa penzi la huyo ambaye haonyeshi kutambua thamani ya penzi lako.

UTUMWA WA MAPENZI

Kipengele hiki ni kama kiini cha mada hii, tunapozungumzia utumwa halisi wa mapenzi, ni pale ulipojitahidi kumshawishi mpenzi huyo, kwa kila njia ili nuweze kuwa naye! Inawezekana ulimshawishi kwa pesa na wakati mwingine, ndugu zake walimlazimisha kuishi na wewe, akaamua ingawa hakupenda.
Mnapokuwa mmeingia kwenye ndoa, hapo sasa ndipo utumwa hukamilika! Sio rahisi kutoka tena (hasa kwa Wakristo) lakini mume/mke huyo atakuonyesha kila aina ya vimbwanga kuthibitisha kuwa hana mapenzi na wewe.
Inawezekana ukahitaji haki yako ya ndoa lakini akawa mgumu kukupa, kwa sababu hakupendi! Alikuoa/olewa na wewe kwa sababu ya shinikizo na sio mapenzi, lakini kwa kuwa tayari unakuwa umeshazoeana naye inakuwa vigumu kumtoa moyoni mwako.
Wengi wao hufikikia hatua ya kuamua maamuzi ambayo sio sahihi, baadhi yao huchanganyikiwa na wengine huona bora kufa kuliko kufedheheka! Kimsingi utumwa wa mapenzi ni ugonjwa mbaya sana kisaikolojia.

CHUNGUZA MOYO WAKE

Hakika utumwa wa mapenzi ni ugonjwa mbaya sana, kimsingi usiruhusu kabisa kuwa mtumwa wa mapenzi. Hilo linawezekana kwa kumchunguza moyo wa huyo umpendaye. Katika hali ya kawaida, ni jambo gumu kidogo lakini iunawezekana.
Unaweza kuuchunguza moyo wake kwa kuangalia je, ni kweli naye anakupenda kama unavyompenda? Kuna wengine hushindwa kukuambia SIKUTAKI, lakini anaendelea kuwa na wewe, kukufanya chombo cha starehe na kukupotezea muda wako. Ni rahisi kumtambua.
Mwulize kwanini anakupenda? Akupe sababu hasa za mapenzi yake kwako, akikuambia anakupenda kwa sababu ya umbo au sura nzuri, tambua huyo sio mpenzi sahihi na huenda akakufikisha katika utumwa wa mapenzi. Anayekupenda, hukujibu kuwa, amekupenda kama ulivyo, anaamini wewe ni mhimnili wa maisha yake na maisha yake yatakuwa kamili akiwa wewe na sio kuzungumzia habari za ngono!
Mara nyingi ukimpigia simu, huchelewa kupokea kwa kisingizio cha kazi nyingi, ukimwandikia sms ndio kabisa hajibu! Yote hiyo ni kwa sababu hakupendi! Hana msisimko wowote na wewe.
Kwanza kama anakupenda, hata kwenye simu yake atakuwa amekuwekea mlio (Ring tone) tofauti na wengine, hivyo ukipiga lazima ajue ni wewe na hata kama ana kazi nyingi kiasi gani anapaswa kupokea, kwa kuwa wewe ni muhimu kwake!

KATAA KUWA MTUMWA

Ukiona niliyoanisha katika kipengele kilichopita, ujue kuwa hakupendi, sasa kama ndivyo, huna sababu ya kukubali kuwa mtumwa! Kataa kwa nguvu na ni bora ukajifunza jinsi ya kukabiliana na hali ya kuishi bila huyo uliyempenda, kuliko kuishi naye halafu akutese.
Vipo vitu vingi vitakavyokusaidia kuepukana na hali ya sononeko katika moyo wako na kuishi maisha yako peke, huku ukimsubiri aliye maalum kwa ajili yako! Kataa kabisa kuwa mtumwa maana maisha yako huweza kuharibika moja kwa moja.

Thursday, March 3, 2011

Hebu angalia hisia nane hatari ili uzikimbie mapema kabla hazijakuharibia penzi lako.


Miongoni mwa vitu vinavyochangia kuharibu uhusiano wa kimapenzi ni hisia. Wapenzi wengi wameachana kwa sababu si kwamba walithibitisha ubaya wa wenzao ila walijijaza wenyewe hisia mbaya na kujikuta wamepoteza thamani ya kupenda. Hebu angalia hisia nane hatari ili uzikimbie mapema kabla hazijakuharibia penzi lako.

1. NASALITIWA
Kuishi katika mapenzi huku ukiwa na fikra kwamba mwenza wako anakusaliti ni jambo baya kwa vile huathiri msukumo wa ndani wa kupenda. Matokeo yake utajikuta ukishindwa kutimiza wajibu wako kama mke/mume kwa sababu tu ya kuendekeza hisia mbaya. Acha kuhisi, tafuta ukweli.

2. TUTAACHANA
Kuna wapenzi ambao wanaishi na mawazo ya “ipo siku tutaachana”. Wanafanya hivyo eti kwa kutafsiri mwenendo usioridhisha wa mapenzi yao. Kusema kweli hili ni jambo baya kwani huondoa ari na kujenga ufa wa mapenzi.
 Huwafanya wapenzi kubakia na wazo moja tu, la kutafuta sehemu mbadala ya kwenda baada ya kuachana. Usiwaze kabisa kuachana hata kama mnagombana na mwenzako kila siku.

3. SIWEZI MAPENZI
Baadhi ya wapenzi huwa na hisia kwamba hawayawezi mapenzi. Hata kama hawajaambiwa chochote kuhusu kutowatosheleza wenza wao  faragha, hukimbilia kujihukumu.

Hujaambiwa kama umecheza chini ya kiwango, hofu ya nini? Usiwaze hivyo, kama una lolote linalokufanya uwe na hofu muulize mwenzio.

4. NINA KASORO
Naamini mitaani wapo watu ambao huamini wana kasoro fulani ndiyo maana hawafikii viwango vya kupendwa kama wanavyohitaji. “Yaani mimi ningekuwa kama fulani ningefurahi sana lakini ufupi wangu ndiyo tatizo.”

Hizi ni hisia mbaya tu, kumbuka kuna wafupi wanapendwa ile mbaya. Jisahihishe na epuka kujishusha hadhi kwenye hisia zako.

5. NITAMUUA
Miongoni mwa hisia mbaya kabisa kwenye mapenzi ni kufikiria kumuua mwenzako kwa sababu yoyote. “Nikimfumania na mwanaume mwingine nitamuua.”

Mtu anayetawaliwa na mawazo ya aina hii anajiweka katika mtego mbaya kisaikolojia wa kuja kutekeleza kile anachojiapiza hata kwa sababu ndogo. Usifikirie hivyo maishani mwako.

6. NIMEKOSEA KUCHAGUA
Usijihukumu makosa kwa sababu umeona mpenzi wako ana tatizo fulani. Fahamu kuwa kasoro ni sehemu ya ubinadamu. Weka mikakati ya kumuongoza mwezio kuliko kuhitimisha kwa mawazo kwamba ulikosea kumchagua. “Ningejua kama yuko hivi nisingemchagua.” Usiwaze hivi!

7. HATUWEZI KUZAA
Kuna wapenzi ambao kwa kuishi miaka mitatu au minne pamoja bila kupata mtoto hufikia kwenye fikra kwamba hawawezi kuzaa. “Mmm, mwaka wa nne umepita bila mtoto, nadhani sisi hatuwezi kuzaa.”

Kwa nini msizae? Hizo ni fikra zako, hamjaambiwa na daktari sasa iweje uwaze hivyo? Jipe moyo kwani kuna watu walizaa baada ya miaka kumi, iweje ninyi wa mwaka mmoja?

8. UNANIDANGANYA
Ipo aina ya watu ambao hata kama wakiambiwa wanapendwa sana, hukimbilia kusema na kuamini kuwa wanadanganywa. “Mmm unanidanganya.” Atasema hivyo licha ya kuona mwanaume anavyojituma kumsotea na kumuonesha kila dalili za mapenzi. Hili ni jambo baya, ukithibitisha kwamba unapendwa usihisi

Unamalizaje migogoro na mpenzi wako?-Sehemu ya kwanza.



RAFIKI zangu, ni imani yangu mtakuwa wazima wa afya na mnaendelea na majukumu yenu vyema. Mimi ni mzima wa afya, nipo hapa kwa ajili ya kuwapa kilicho bora zaidi katika uhusiano na wapenzi wetu.

Nawashukuru wote ambao mmekuwa mkiwasiliana nami kwa njia mbalimbali, simu, sms, waraka pepe na katika ukurasa wangu wa Facebook. Ushauri na maoni yenu yananitia nguvu.

Leo tunaangalia mada muhimu sana katika mapenzi, nachambua juu ya migogoro ambayo inaweza kutokea kati yako na mwenzio, je, unaimalizaje? Unajua katika uhusiano wowote, lazima wakati mwingine kutokee kutokuelewana, vivyo hivyo katika uhusiano wa mapenzi lakini tatizo si migogoro, bali ni jinsi gani unavyoweza kutatua migogoro uliyonayo.

Hebu jibu swali hili, umewahi kugombana, kulumbana au kuwa na migogoro na mpenzi wako? Jibu lako litakuwa mwanga wa kuwa na uelewa wa kutosha katika vipengele vinavyofuata. Sasa tuanze moja kwa moja kwa kufahamu maana ya migogoro na malumbano.

Maana yake ni nini hasa?
Naweza kuita mgogoro, malumbano au ugomvi. Ni maneno matatu yenye maana zinazokaribiana, ingawa ukweli ni kwamba yana maana tofauti kidogo! Mnaweza kuwa na mgogoro na mwenzi wako lakini yasiwepo malumbano.

Kwamba inawezekana mpenzi wako amekukosea na ukawa mwanzo wa migogoro katika penzi lenu, lakini kutokana na uelewa wako na kukubali kosa mapema ikiwa ni pamoja na kuomba radhi, kukawa hakuna malumbano na mambo yakawa sawa.

Wakati huo huo, kunaweza kukawa na tatizo linaloweza kusababisha migogoro ambayo huzaa malumbano na mwisho wake ni ugomvi! Naamini tunakwenda sawa!

Kwa nini nimeeleza hayo? Nataka twende sawa, hatua kwa hatua katika mada hii ambayo naamini ni tatizo kwa wengi walio katika uhusiano. Baada ya kuona maana ya maneno matatu muhimu ambayo kwa hakika yanakaribiana, ambayo tunayajadili katika mada yetu ya leo, sasa tuone jinsi matatizo hayo yanavyotokea.

Chanzo cha tatizo
Migogoro ambayo nimeainisha hapo juu, haiwezi kutokea bila kuwa na vyanzo. Lazima kuna mambo ambayo yametokea kwanza, kabla ya tatizo husika kukua na mwisho wake kuanza migogoro, malumbano kabla ya ugomvi.

Kama wahusika hawatakuwa makini, mwanzo wa ugomvi ni mwendelezo wa kuachana hapo baadaye, jambo ambalo mwenye mapenzi na akili timamu hawezi kukubali likachukua nafasi. Hebu sasa pitia mambo hayo.

Penzi kupungua!
Yapo mengi ambayo husababisha migogoro katika mapenzi lakini kubwa zaidi ni kuchuja au kupungua kwa penzi. Unapokuwa na mwenzi wako, halafu kwa sababu ambazo unazijua mwenyewe unajikuta penzi limepungua, huo unaweza kuwa mwanzo wa migogoro.

Kila atakachokiongea utaona kero, kila wakati utakuwa mtu wa kukasirika na usiyependa kufuatwafuatwa! Katika upande mwingine, kama mwenzi wako amejikuta akiingia katika ushawishi na penzi lake kwako kupungua, ni mwanzo wa kuwa na mawasiliano mabaya na wewe, ambayo bila shaka lazima yatasababisha migogoro ambayo huzua malumbano kabla ya ugomvi.

Utashangaa mpenzi wako anakununia bila sababu za msingi, hana raha na wewe, hataki mzungumze chochote kuhusu penzi lenu, hapo ujue ni mwanzo wa migogoro.
Matatizo binafsi...

Hili pia linaweza kuwa chanzo cha ugomvi katika maisha ya wapendanao. Mathalani mwenzi wako ametoka kazini akiwa na matatizo binafsi kichwani, wewe kwa kutokujua unaanza kumuuliza kwa ukali.

Hebu soma mfano ufuatao; “Unakuja nyumbani umenuna, sijui una matatizo gani? Ndiyo yale yale, ugombane na wanawake zako huko nje, halafu unakuja kuninunia hapa nyumbani.” Hii ni moja kati ya kauli mbaya sana kwa mpenzi wako kabla ya kujua sababu ya ukimya na upole aliokuja nao.

Yawezekana ana matatizo binafsi, kwa nini uanze kumhisi vibaya? Tulia, fikiria kwa makini kabla ya kutamka chochote kwa mpenzi wako.

Msongo wa mawazo!
Kipengele kilichopita, hakina tofauti kubwa sana na hiki. Matatizo binafsi ni mwanzo wa kuwa na msongo wa mawazo. Pengine mambo yamemwendea kombo, amegombana na rafiki yake wa karibu, ameharibu kwa bahati mbaya mali ya kampuni n.k.

Mambo haya na mengine yanayofanana na hayo, yanaweza kusababisha mtu kuwa na msongo wa mawazo ambao utasababisha ashindwe kuwa na mawasiliano mazuri na wewe.

Kupungua kwa mawasiliano bora baina ya wapenzi ni mwanzo wa ugomvi, kwani kila mmoja atajiona yupo sahihi kwa sababu mwenye msongo wa mawazo anaamini njia sahihi ni kutulia au kujifungia chumbani akiwaza atakavyotoka katika matatizo yake, wakati anayetengwa na kununuwa ataamini mpenzi wake amepunguza mapenzi kwake.

Majibizano yake ambayo kwa hakika siku zote huwa hasi, ni chachu ya kuruhusu migogoro, malumbano kabla ya ugomvi kutokea. Mwanzo huo kama busara haitachukua nafasi, Kuachana ndiyo kitu pekee ambacho kinaweza kuchukua nafasi kwa wakati huo.

Unamalizaje migogoro na mpenzi wako? -2


NINA furaha sana moyoni mwangu kukutana nanyi tena wapenzi wasomaji wa safu hii namba moja kwa mada za mapenzi na uhusiano nchini. Bila shaka mmekuwa mkijifunza mambo mengi na kubadilika. Karibuni tena katika mwendelezo wa mada yetu iliyoanza wiki ya jana.
Hebu tuendelee kuona vyanzo hivyo kabla ya kwenda katika dawa yenyewe. Tuingie darasani!

Kutetereka kimaisha
Hili nalo huchangia ingawa siyo kwa kiasi kikubwa sana. Kushuka kimaisha ni hali ya kawaida ambayo huweza kumpata mtu yeyote aliye chini ya jua, lakini utafiti wa wanasaikolojia ya Uhusiano wanasema kwamba, kushuka kimaisha ni kati ya sababu zinazosababisha kuporomoka kwa hisia halisi za mapenzi.

Tatizo hili huwakumba zaidi wale ambao wapo katika uhusiano wa karibu zaidi waliooana au hata wanaoishi pamoja kwa muda mrefu.

Mwanasaikojia George K. Pollyns wa Ujerumani katika kitabu chake cha Love Season, anaelezea kushuka kimaisha kama mwanzo wa ugomvi ndani ya nyumba kutokana na furaha iliyokuwepo mwanzo kupunguzwa na ukali wa maisha.

“Lakini hata hivyo, penzi imara haliwezi kuyumbishwa na ukali wa maisha, maisha na mapenzi yanakwenda sanjari, lakini fedha na mapenzi yanatofautiana ingawa pia maisha na fedha ni kama ndugu.

“Umakini ni kitu cha kwanza kabisa kwa walio kwenye uhusiano ukizingatia ukitetereka kidogo tu, unaruhusu mwanya wa kuachana kuingia kati yenu,” ndivyo inavyoeleza sehemu ya nukuu katika kitabu hicho.

Naye Mwanasaikolojia Richard Manyota wa Tanzania, katika kitabu chake cha Saikolojia na Maisha, anaeleza kwamba, pamoja na kuwa ukali wa maisha ni chanzo cha kupungua kwa mapenzi, lakini yeye haamini sana katika hilo, ikiwa wapenzi hao wana mapenzi ya dhati mioyoni mwao.

“Ukiona hayo yanayotokea, basi ujue penzi la awali halikuwa la asili, unajua wengi wanashindwa kutofautisha, penzi la dhati na tamaa ya muda, hili ndiyo tatizo kubwa!” Sehemu ya nukuu katika kitabu chake hicho inaeleza.

Bila shaka, maoni ya Pollyns na Manyota yanaweza kukufanya ujifunze kitu fulani na kuwa na kitu kipya katika ufahamu wako juu ya maisha ya uhusiano, mapenzi na ndoa.

Kutojaliana
Kupungua kwa mapenzi na kutokumjali mwenzi wako, kunatajwa kama moja ya sababu za kuanzisha malumbano. Hili halina ubishi, kwani kama umezoeshwa na mpenzi wako kutoka kila mwishoni mwa wiki, halafu ghafla ratiba zinabadilika, lazima kutakuwa na matatizo.

Tatizo huanza pale mwenzi wako atakapokuuliza sababu za kubadilisha ghafla ratiba ambapo bila shaka hutakuwa na jibu yakinifu, hali itakayozusha ugomvi. Ni vizuri wapenzi wakapendana kwa dhati, kujaliana na kupeana taarifa mapema za mabadiliko yoyote ambayo yametokea.

Mathalani haupo sawa kiakili au umeyumba kidogo kimapato, basi ni vizuri  ukamwambia mpenzi wako kwa sauti tamu ya upole: “Sweetie hali mbaya, mifuko imetoboka, wiki hii hatutaenda mahali popote. Itabidi tutulie nyumbani.”

Kauli kama hiyo, lazima mwenzi wako atakuelewa na kwa kiasi kikubwa mtakuwa mmeepusha migogoro ambayo si ya lazima. Lazima wewe uwe wa kwanza kuhakikisha kwamba unalinda uhusiano wako usiingie kirusi cha migogoro. Inawezekana kabisa rafiki zangu. 

POKEA, KUBALI TATIZO
Hakuna haja ya papara wala hasira, matatizo katika uhusiano ni jambo la kawaida ambalo kiukweli unatakiwa kujiandaa kukabiliana na changamoto hizo.

Kubali tatizo, kisha tulia na panga jinsi ya kulimaliza kwa njia bora zitakazouacha uhusiano wako katika hali nzuri. Kwanini ubadilishe wapenzi kila kukicha? Unatafuta nini? Upe ubongo wako nafasi ya kufikiri.

Maamuzi ya hasira au kukomoa mwisho wake huwa ni machozi, epuka machozi ambayo hayana sababu. Siku zote, ukikubali kosa na kulipokea, ni mwanzo mzuri wa kuelekea kwenye kutafuta njia za utatuzi.

UNATATUAJE?
Hapa ndipo umakini wa kiwango cha juu kabisa unapohitajika. Jinsi gani unamaliza matatizo yako? Unatumia ubabe au utaratibu?
Kama nilivyoeleza awali, wapo ambao wanaamini katika ukali na ukorofi, vitu ambavyo siyo tiba ya kweli.

Baadhi ya watu wanaamini wakitumia ukali sana, wanawapa wapenzi wao nafasi ya kubadilika na kueleza chanzo cha matatizo waliyonayo. Hili halina ukweli hata kidogo.
Kipengele kifuatacho, ikiwa utakipitia kwa umakini litakuwa ni dirisha lako lenye uwazi mkubwa wa kukuelekeza kwenye mafanikio na kukuacha salama  kwenye uhusiano wako.

NJIA SALAMA
Pamoja na matatizo niliyoyaeleza hapo juu, wakati mwingine inawezekana kabisa mwenzi wako akawa ndiye mwenye matatizo, lakini kwa kushindwa kwako kuwasilisha vyema hisia zako, ukaharibu! Dondoo hizi zitakufaa sana katika utatuzi wa migogoro katika uhusiano wako.

(i)Zungumza kwa upole
Hii ni hatua ya kwanza kabisa katika kuelekea kuutafuta ukweli. Kwa kutumia upole, hatakuogopa na ataona wewe ndiye kimbilio lake.

Mwulize taratibu kama alikuwa na matatizo yoyote kikazi au kuna mahali ulimkwaza. Tabasamu lako linatakiwa kuwa silaha ya kwanza. Atasema tu!

(ii)Kuwa mdadisi
Kwa kutumia sauti ile ile ya upole kama nilivyoeleza katika kipengele hicho hapo juu, mdadisi! Kuwa mdadisi kwa kutumia ucheshi wa kila aina.

Kama utamdadisi taratibu, kauli yako na upole wako vitakuwa mwanga wa yeye kukueleza ukweli wa kinachomsumbua. Lazima mwisho  atakueleza ukweli.
 
IBUKA MSHINDI
Kwa kuzingatia vijisehemu nilivyoviainisha hapo juu, lazima atasema kinachomsumbua. Kujua tatizo ni mwanzo mzuri wa kuelekea kwenye utatuzi.

Jadili tatizo hilo, kisha endeleeni na maisha yenu kama kawaida. Fahamu kwamba, migogoro katika mapenzi ni jambo la kawaida na unachotakiwa kufanya ni kuwa na moyo wa subira na kufuata taratibu zilizopendekezwa bila kukosea hata moja.