Wednesday, April 27, 2011

Wengi wanapoteza mvuto, wanaachwa kwa sababu hawajitambui


Hakuna mtu ambaye hapendi kuonekana bora katika mapenzi. Ibuka wewe ili uwe wa kwanza kutamka kuwa unajisikia furaha mwenzi wako anapokudharau. Yaani anapokushusha thamani kwamba hujiwezi kunako duru la mapenzi.

Kimsingi, tunakubaliana kuwa kila mmoja wetu anapenda kuonekana hodari katika kumtosheleza mwenzi wake. Hivyo basi kasoro ndogo ndogo ambazo zinatukuta baadhi yetu huwa zinakera kama siyo kuumiza. Kamusi ya mtaani inasema “zinakata stimu.”

DAWA NI NINI?
Uponyaji katika saikolojia si kama kikombe cha Babu wa Loliondo. Kadhalika tiba yake haishabihiani na mtindo wa dozi kama ambavyo mgonjwa wa malaria hupewa hospitali. Ukienda kwenye mitishamba ndiyo unapotea njia kabisa.

Ukitoka kupona kisaikolojia, kwanza kabisa unatakiwa ujitambue wewe mwenyewe. Matawi ya kujitambua ni kwamba unapaswa kujua udhaifu wako binafsi na eneo ambalo wewe unaamini kwa asilimia 100 kwamba wewe ni hodari.

Mweledi katika elimu ya saikolojia ni yule ambaye anatumia kwa nguvu na ujasiri lile eneo ambalo yupo ngangari kwa lengo la kuficha udhaifu unaomkabili. Mfumo huo hata kwenye mapenzi upo, ukiutumia utamkosha mwenzi wako.

Mathalan, unajigundua kuwa wewe huna uwezo wa kusafiri kwa muda mrefu (nazungumzia safari ya faragha) lakini wakati huo huo, unajikubali kwamba kwenye eneo la kumpandisha wazimu mwenzi wako, upo juu kupita Mlima Kilimanjaro.

Unapolibaini hilo, unapaswa kuweka pembeni tamaa ya kuwahi kukwea na kulalia tuta, badala yake unatumia maarifa yako kumshambulia kitaalamu, unacheza na maeneo yanayompa ‘wehu flani’ hadi uhakikishe anakuwa hoi bin taaban.

Matokeo ya mashambulizi yako ni kwamba anapokuwa hoi, maana yake hisia zake zimekaribia kwa kiwango kikubwa, hivyo hata pale unaporidhika na kuanza zoezi la juu ya tuta, ‘pushapu’ hazitakuwa nyingi kabla ya safari kufika mwisho wa reli.

Ujanja huo unaweza kukufanya utembee kifua mbele mitaani. Kipi kinachokusononesha? Ukiwa faragha mwenzi wako anakiri kwamba kwenye kila safari yenu, siku zote humfikisha kule ambako anapataka na pengine aliyekutangulia alikuwa anamuacha njiani.

ANGALIZO; Unapoanza safari ya faragha na mwenzi wako, hakikisha anafika kule panapotakiwa (mwisho wa safari). Ukimuacha njiani, unampa mateso makubwa. Inawezekana una nguvu kidogo, hilo siyo tatizo, tumia akili na maarifa kushinda mchezo.

Ni elimu ya kujitambua. Kuna mwanasaikolojia mmoja aliwahi kuandika: “Mtu anayefanikiwa kubaini tatizo sugu linalomsumbua, anayejua udhaifu wake, huyo ni bora zaidi kwa maana ataishi kwa kuuficha udhaifu wake ili usimharibie.”

Hapo hapo naongeza kuwa mtu bora kwenye mapenzi ni yule anayeamua kuishi kwa kuweka mbele uimara wake na kuuficha udhaifu wake. Anafanyia kazi pande zote mbili zilizomo ndani yake, halafu anatengeneza sura yake namba moja ambayo itambeba siku zote.

Kinyume cha kutojitambua ni kugeuka mzigo kwa kila unayekuwa naye. Kilichomkimbiza kwa wa mwaka jana wa mwaka huu naye anakikuta, kwa hiyo hakai. Utakimbiwa na wangapi? Kubadilisha wapenzi kila mara jamii haitakuelewa, itakuona ‘si bure’.

Kwa kifupi ni kwamba kila udhaifu unaoweza kuwemo ndani yako, ujue kuna tiba mbadala. Muhimu ni kubeba tatizo kwa umakini mkubwa halafu uamue kuchukua hatua za kulimaliza. Ni busara kutambua kiini chake kisha uanze kufanya kile kinachostahili.

Wanasema, “Yako duh! Ya wenzako midomo juu!” Kwamba unakuwa maridadi kutambua kasoro za mpenzi wako ilhali wewe mwenyewe unavumiliwa sana. Anza kujisafisha kwa kiwango kinachotakiwa, baada ya hapo tekeleza mengine.

Kuna stori hii: “Benjamin baada ya kukimbiwa na wanawake wawili, alikuja kugundua kwamba tatizo lililokuwa linamsumbua mpaka kukimbiwa na wenzi wake ni maumbile yake ya siri. Alijaliwa maumbile makubwa mno.

“Bahati mbaya alikuwa hajitambui, kwa hiyo akawa anatumia nguvu akiwa faragha, hivyo kuwasababishia maumivu na mateso kama si karaha badala ya raha, wanawake ambao alikuwa akikutana nao.”

No comments: