Thursday, May 10, 2012
Namna ya kuvaa jioni kulingana na umbo lako
KWA kawaida kila mwanamke hutamani kuwa na mvuto wa kutosha hasa anapotoka nyakati za jioni.
Hata hivyo kuna baadhi ya wanawake wanashindwa kufahamu wavae nguo za aina gani ili wawe na mvuto huo kulingana na shepu zao.
Makala haya yanaeleza aina ya nguo ya mhusika kulingana shepu yake.
Mfupi na mwembamba
Usifanye makosa kwa kuvaa gauni ambalo ni kubwa. Jaribu kuepuka magauni marefu au sketi ndefu. Badala yake vaa nguo fupi ambazo zitaonyesha miguu yako, hapo angalau utaonekana �umejazia�.
Vaa viatu virefu iwezekanavyo ili uonekane mrefu.
Kujazia juu na chini (Pear-Shaped)
Kama mwili wako umejaaliwa kujazia juu na chini yaani hipsi kubwa na kifua kipana, utapendeza katika nguo ambayo itakufanya uonekane na kifua chembamba na pia itakayokushika hipsi zao.
Jaribu kuvaa mkanda ulionakshiwa na madini ya fedha au rangi ya dhahabu ili kiuno kionekane.
Kujaa kote (Apple Shape)
Hii ni shepu ambayo mtu anakuwa na makalio manene, tumbo nene, mgongo mpana na kifua kipana. Mtu wa namna hii anatakiwa kuvaa gauni lenye mikono kidogo na lililoungwa chini kidogo ya matiti.
Gauni hilo litaficha tumbo mikono na matiti. Nguo yenye shingo ya �V� inaweza kukufanya uonekane mwembamba kiasi. Lakini pia usiogope kuonyesha miguu yako kwa kuvaa gauni fupi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment