Tuesday, September 7, 2010

UMFANYEJE HUYU?

UMFANYEJE HUYU? NIMWAMINI AU?

Mpo kwenye luv ndan ya mwezi tu,lakini unapokea sms ya mpenzio iliyopaswa kutumwa kwa mwingine bahati mbaya ikaingia kwako.inaonyesha aliye kusudiwa ni mpenziwe.unamuuliza ni vip?anakwambia ni rafiki yake alituma kwa mkewe,kwakutumia simu yake.mpo long distance relationship.

SOMA WALIYOJIBU WENZIO


Pole dada. Huyo hanaukweli hiyo ndio tabia ya sisi wanaume wengi hua hivyo ila usimmwage kwanza endelea kumchunguza na utaupata ukweli tu. Ingawaje hukutuambia uko nae muda gani. Kwanza endelea kumuamini huku ukichunguza. - Suma. Znz.



usiwe na hofu dada ni rahisi sana, ni kweli kuna wasichana wengi kama wewe wanajiuliza ni kwa nini hata salam hawapati kutoka kwa wanaume na wengine wanashindwa hata kupata wa kuweza kufunga ndoa huku miaka ikizidi kwenda.
Kuna siri ndogo sana wengi huwa hawaitambui.
niandikia kwa email yangu hii (be_kind_rewind08@yahoo.com) nikupatie namna unatakiwa kufanya katika mambo yako ya kila siku, ni rahisi na hautaweza kuamini hakuna uchawi wowote katika mapenzi - Mike



..taa nyekundu imewaka dadangu...kaa barabarani ugongwe na gari....huyo mpenzio ni muongo mkubwa...Haiwezekani rafiki yake atumie sim yake alafu na namba aweke yako...INAKUJA HIYO?kwanza pima hilo lisms...alafu mwambie SIDANGANYIKI.....Anakumaliza huyo fataki...ana mpenzi mwingine tayari...atakuletea ngoma huyo!sepa - herbert stylz



du unangoja nini kama ndo ndani ya mwezi tu unaona vituko namna hii je mkimaliza mwaka si utakua ushazimia?? mmwage huyoo tapeli wa malove - pendo



Hayo yamedhihirika mapema kabla hamjafika mbali ili usije jutia uamuzi wako kwa uliyempenda. Si rahisi kwa ulimwengu wa sasa Mtu kutuma sms ya mapenzi kwa mpenziwe kwa simu ya rafiki yake. Sikushauri Muachane sasahivi ila kaa kwa tahadhari huku ukimwomba Mungu, na pia usikubali kushiriki tendo la ndoa pengine ndiyo nia yake ili apate kukuacha baada ya kukuchezea. - Venance Mattei



hatujui umefika kiasi gani kwa huyo mpenzi wako ingawa ni mwezi tu,kikubwa ni kufatilia nyendo zake, ili ujue kweli wa sms ile, ila kwa jinsi ulivyojieleza; mpenzi wako hajatulia,haiwezekani simu atumie mtu mwingine halafu sms ije kwako,ila simu ikiwa yako mwenyewe ni rahisi kuchanganya mambo mana unaweza kumtumia hata mzazi usipoangalia.... - mdau

No comments: