Tuesday, September 7, 2010

FAHAMU NJIA YA KUREFUSHA NYWELE WADADA........

Fahamu njia rahisi ya kurefusha nywele
Na NICO TRAC

MARA nyingi, wanawake hukatika nywele kutokana na kushindwa kuzihudumia vema au kutokana na kukumbana na hali mbaya ya hewa.

Katika makala ya leo tutaangalia mbinu ya kuhakikisha nywele zanakuwa na afya wakati wote.

Kitu cha kwanza cha kufanya ni kutumia mafuta aina ya 'Biotin', ambayo kwa kawaida huongeza vitamini katika ukuaji wa nywele.

Vilevile muhusika anatakiwa kuongeza asali kwenye 'conditioner' na kupaka kichwani angalau mara moja kwa wiki.

Wakati muhusika anapopaka mchanganyiko huo anatakiwa kukaa kwa dakika 30, kuhakikisha vitamini inaingia vema kwenye nywele. Iwapo muhusika atakosa asali anaweza kutumia parachichi.

Kitu kingine kinachoweza kumsaidia mwanamke akuze nywele ni kujitahidi kuepuka kukaa katika mashine ya kukaushia nywele mara kwa mara.
Muhusika anaweza kukausha nywele kwa kutumia 'drier' mara moja kwa wiki.
Vilevile mtu anaweza kuzuia ukatikaji wa nywele kwa kuepuka kuchana nywele kwa kutumia kitana chenye meno madogo wakati nywele zikiwa na maji.

No comments: