Wednesday, September 15, 2010

Mpangala: Nilitaka kumzuia asishiriki Miss Tanzania

Genevive Mpangala Miss Tanzania 2010.
Na Ahadi Kakore
BABA mzazi wa Miss Tanzania 2010, Genevieve Mpangala, Emmanuel Mpangala amesema nusura amzuie mwanaye kushiriki mashindano hayo ya urembo kutokana na hofu kuwa huenda akaharibikiwa.

Akizungumza na Championi Jumatano, Mpangala alisema anampongeza mwanaye kwa ushundi huo ingawa, alikuwa akisita kumruhusu kushiriki.

“Nilikuwa sitaki lakini baadaye nikafikiria, nikaona inawezekana nikamkataza mtoto kufanya maamuzi yake ambayo ni sahihi. Hivyo, mimi na mama yake tuliamua kumruhusu na kumpa baraka zote.

“Najua kwa sasa ameingia kwenye ulimwengu wa watu maarufu hivyo atakuwa akimulikwa na vyombo vya habari, naamini ataendelea kuwa mwema katika jamii hasa ikizingatiwa kuwa bado umri wake ni mdogo. Nasi wazazi tutaendelea kumshauri juu ya maisha yake mapya,” alisema Mpangala ambaye ni Meneja wa timu ya Yanga.

Tayari Mpangala ametangaza kumpa mwanaye nyumba anayomiliki iliyo katika kitongoji maarufu cha jiji la Dar es Salaam kama zawadi na pongezi kutokana na kutwaa taji hilo.

Genevieve, mtoto wa pili katika familia ya Emmanuel na Maria Mpangala alikuwa Miss Chang’ombe na kutwaa taji la Kanda ya Temeke kabla ya kutwaa taji la Miss Tanzania wikiendi ilyopita.

Warembo wengine wa Temeke waliowahi kutwaa taji hilo tokea kuanzishwa kwake mwaka 1994, ni Happiness Magese (2001) na Sylvia Bahame (2003).

No comments: