Hii ina maana pana sana , lakini naweza kutoa moja kama mjumuisho wa yote! Utumwa wa mapenzi unaweza kutokea pale, utakapompenda mtu ambaye hana habari na wewe kabisa, yaani unajikuta ukioza juu yake, lakini anakuwa hana mapenzi na wewe kabisa.
Wakati mwingine unaweza ukamshawishi mtu huyo kwa vitu fulani, akakubali kuwa na wewe lakini sio kwa mapenzi ila kwa kuwa kuna kitu fulani atapata kutoka kwako.
Muda mwingi utautumia kufikiri kwanini fulani hakuipendi? Una kasoro gani n.k, kimsingi kama ukiruhusu utumwa wa mapenzi, mpangilio wa maisha yako unaweza kuharika na kukosa muelekeo kabisa.
UTAJUAJE KAMA WEWE NI MTUMWA?
Hili ni rahisi kutambua ingawa ni hatua mbaya sana katika maisha yako. Jambo la kwanza ni mabadiliko ya hisia za moyo wako, utajikuta ukimpenda mtu sana , ambaye hata time kabisa na wewe! Pamoja na kuwa anaonyesha kila dalili za kukuchukia lakini bado utahisi kumpenda na kumhitaji katika maisha yako.
Moyo wako huendele kuysisitiza kuwa huyo sio sahihi kwa maisha yako, lakini bado mtu huyo ataendelea kukuonyesha kila vibwanga vya kuchukiza. Sio jamboi la ajabu kuhiusi kufa kuliko kuendelea kuteseka kwa penzi la huyo ambaye haonyeshi kutambua thamani ya penzi lako.
UTUMWA WA MAPENZI
Kipengele hiki ni kama kiini cha mada hii, tunapozungumzia utumwa halisi wa mapenzi, ni pale ulipojitahidi kumshawishi mpenzi huyo, kwa kila njia ili nuweze kuwa naye! Inawezekana ulimshawishi kwa pesa na wakati mwingine, ndugu zake walimlazimisha kuishi na wewe, akaamua ingawa hakupenda.
Mnapokuwa mmeingia kwenye ndoa, hapo sasa ndipo utumwa hukamilika! Sio rahisi kutoka tena (hasa kwa Wakristo) lakini mume/mke huyo atakuonyesha kila aina ya vimbwanga kuthibitisha kuwa hana mapenzi na wewe.
Inawezekana ukahitaji haki yako ya ndoa lakini akawa mgumu kukupa, kwa sababu hakupendi! Alikuoa/olewa na wewe kwa sababu ya shinikizo na sio mapenzi, lakini kwa kuwa tayari unakuwa umeshazoeana naye inakuwa vigumu kumtoa moyoni mwako.
Wengi wao hufikikia hatua ya kuamua maamuzi ambayo sio sahihi, baadhi yao huchanganyikiwa na wengine huona bora kufa kuliko kufedheheka! Kimsingi utumwa wa mapenzi ni ugonjwa mbaya sana kisaikolojia.
CHUNGUZA MOYO WAKE
Hakika utumwa wa mapenzi ni ugonjwa mbaya sana , kimsingi usiruhusu kabisa kuwa mtumwa wa mapenzi. Hilo linawezekana kwa kumchunguza moyo wa huyo umpendaye. Katika hali ya kawaida, ni jambo gumu kidogo lakini iunawezekana.
Unaweza kuuchunguza moyo wake kwa kuangalia je, ni kweli naye anakupenda kama unavyompenda? Kuna wengine hushindwa kukuambia SIKUTAKI, lakini anaendelea kuwa na wewe, kukufanya chombo cha starehe na kukupotezea muda wako. Ni rahisi kumtambua.
Mwulize kwanini anakupenda? Akupe sababu hasa za mapenzi yake kwako, akikuambia anakupenda kwa sababu ya umbo au sura nzuri, tambua huyo sio mpenzi sahihi na huenda akakufikisha katika utumwa wa mapenzi. Anayekupenda, hukujibu kuwa, amekupenda kama ulivyo, anaamini wewe ni mhimnili wa maisha yake na maisha yake yatakuwa kamili akiwa wewe na sio kuzungumzia habari za ngono!
Mara nyingi ukimpigia simu, huchelewa kupokea kwa kisingizio cha kazi nyingi, ukimwandikia sms ndio kabisa hajibu! Yote hiyo ni kwa sababu hakupendi! Hana msisimko wowote na wewe.
Kwanza kama anakupenda, hata kwenye simu yake atakuwa amekuwekea mlio (Ring tone) tofauti na wengine, hivyo ukipiga lazima ajue ni wewe na hata kama ana kazi nyingi kiasi gani anapaswa kupokea, kwa kuwa wewe ni muhimu kwake!
KATAA KUWA MTUMWA
Ukiona niliyoanisha katika kipengele kilichopita, ujue kuwa hakupendi, sasa kama ndivyo, huna sababu ya kukubali kuwa mtumwa! Kataa kwa nguvu na ni bora ukajifunza jinsi ya kukabiliana na hali ya kuishi bila huyo uliyempenda, kuliko kuishi naye halafu akutese.
Vipo vitu vingi vitakavyokusaidia kuepukana na hali ya sononeko katika moyo wako na kuishi maisha yako peke, huku ukimsubiri aliye maalum kwa ajili yako! Kataa kabisa kuwa mtumwa maana maisha yako huweza kuharibika moja kwa moja.
No comments:
Post a Comment