Saturday, April 7, 2012

BREAKING NEWS: STEVEN KANUMBA AMEFARIKI DUNIA.

TULIKUPENDA STEVEN KANUMBA THE GREAT LAKINI MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI, PUMZIKA KWA AMANI BRO, UMETUTANGULIA MBELE YA HAKI, SISI TUKO NYUMA. DUNIANI TUPO SAFARINI. REST IN PEACE STEVEN KANUMBA
 Msanii maarufu nchini Steven Kanumba amefariki dunia ghafra na maiti iko mochwari muhimbili. Habari zaidi kuwajia…


Taarifa nilizozipata sasa hivi kutoka kwa mwigizaji Dino, ni kwamba kweli mwigizaji STEVEN KANUMBA amefariki dunia na inaaminika chanzo cha kifo chake ni baada ya kuanguka na kuanza kutoa mapovu hapohapo nyumbani kwake, alikua akiishi na mdogo wake anaitwa Fetty aliekua chumba kingine ambae amethibitisha kweli kwamba alimkuta kaka yake akiwa ameanguka.

Polisi wameondoka nyumbani kwa Kanumba muda mfupi uliopita baada ya kuwachukua waliokua wanaishi na Kanumba akiwemo mdogo wake Fetty ili kwenda kusaidia maelezo ya kilichotokea.

Bado watu wanazidi kuongezeka nyumbani kwa Kanumba ambapo tayari idadi kubwa ya wasanii wenzake wamefuka pamoja na watu mbalimbali, Mtandao huu utaendelea kukufahamisha kinachoendelea kadri taarifa zitakavyozidi kupatikana.

Ila kumekua na taarifa nyingine ambazo hazijathibitishwa kwamba Kanumba alianguka na kuumia kichwani baada ya mpenzi wake kumsukuma na kuanguka wakati wanagombana. 

No comments: