Washiriki wa kitongoji Kanda ya kaskazini,Miss Arusha City Center 2012, wakiwa katika picha ya pamoja,tayari kuchuana vikali Mei 5 2012 ndani ya hoteli ya Kitalii,Naura Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.katika shindano hilo kiingilio kimepangwa kuwa ni kwa viti maalum ni sh.25,000/= na kwa viti vya kawaida ni sh 15,000/=
Washiriki wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo yatolewayo na chuo cha Udereva na Ufundi,Modern Driving School,ambao pia ni moja ya wadhamini wa shindano hilo.
Washiriki wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa darasani kwenye mafunzo ya nadharia yatolewayo na chuo cha Udereva na Ufundi,Modern Driving School,ambao pia ni moja ya wadhamini wa shindano hilo.
Mashindano
ya Ulimbwende ngazi ya kitongoji Kanda ya kaskazini,Miss Arusha City
Center 2012,yanatarajiwa kufanyika Mei 5 2012 ndani ya hoteli ya
Kitalii,Naura Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.
Akizungumza leo jijini Arusha,Mratibu wa shindano hilo Bi Upendo
Simwita kutoka kampuni ya Tour Visual Entertainment ambao ndio waandaji
wa shindano hilo,amebainisha kuwa mpaka sasa maandalizi yao yanakwenda
vizuri na kila kitu kimekwisha kamililka ikiwemo sambamba na kuwapata
warembo ambao mpaka sasa wametimia 20.
Bi Upendo Simwita amesema kuwa wameishakamilisha mchakato wa kuwapata
Warembo wenye mvuto na wenye vigezo stahiki,anaongeza kuwa warembo hao
wenye ari kubwa ya ushindani,kama waandaji watahakikisha muwakilishi wa
Miss Tanzania 2012 anatokea kwenye kitongoji hicho.
“Shindano hilo litakalokuwa la tofauti kubwa na miaka ya nyuma
litawakutanisha walimbwende wapatao 20,ambao watachuana vikali jukwaani,
na hatimaye kumpata Mshindi wa Miss Arusha City Center”,alisema
Upendo.Amesema kuwa kiingilia katika shindano hilo kimepangwa kuwa ni
kwa viti Maalum sh 25,000/= na kwa viti vya kawaida sh.15,000/=. Fanya
booking yako ya tiketi mapema kupitia namba – 0755975454 au 0713681059.
Kwa upande wa Burudani,Upendo amesema kuwa kutakuwepo na Msanii
mahiri wa Muziki wa kizazi kipya aitwaye Sam wa Ukweli,Muziki wa
Asili,Live Band ya Watoto wa Simba pamoja na burudani nyingine
mbalimbali zitakazotolewa na walimbwende wenyewe siku hiyo.
Upendo amewataja wadhamini wa shindano hilo kuwa ni REDD’S
ORIGINAL,NAURA SPRINGS HOTEL,CLAUDS FM / CLAUDS TV AND MAWINGU CLUB –
ARUSHA,BG HORIZON, MODERN DRIVING SCHOOL,MAKO ADVENTURE,SEBE & BEKI
FOR LIFE, MWANDAGO INVESTMENT,S.G. RESORT,MEJA LINK LTD,GEO
SECURITY,GOLDEN ROSE HOTEL,RIVERSIDE SHUTTLE SERVICES,ARUSHA TRAVEL
LODGE,LITTLE ROSES, LA BELLA VISTA,WAKIPAMBWA NA JANETH BEAUTY PAURLOR
NA BI. HADIJA HASSAN.
No comments:
Post a Comment