MAMBO MACHACHE YA KUYAFAHAMU ILI KUEPUKA KUSALITIWA
1.Amini hawezi kukusaliti
Jambo la kwanza kabisa ni kujenga imani kwamba mpenzi wako anakupenda,
anakuheshimu na kukuthamini hivyo hawezi kushawishika kwa namna yoyote
ile kukusaliti.
Hii itakufanya
kuwa na furaha na yeye, pia utamfanyia mambo ya kumfurahisha. Ukiwa huna
imani na mpenzi wako, unaweza kujikuta unapunguza mapenzi kwake na
matokeo yake ukachochea yeye kuanza kukusaliti.
2.Mtosheleze
Mpenzi wako mchukulie kama mtoto. Unapomlisha unahakikisha ameshiba
ndiyo unamuacha. Akitaka pipi unamnunulia. Vivyo hivyo kwa mpenzi wako.
Mtoshelezea katika kila nyanja.
3.Muoneshe upendo wa hali ya
juu, mpe heshima anayostahili na pale mnapokuwa kwenye mambo yetu yalee,
mpe hadi aseme nimeshiba mpenzi wangu. Ukifanya hivyo aende nje
kutafuta nini? Akienda, huyo ana tamaa zake za kijinga na ukibaini
muache haraka.
4.Zungumza naye
Ndiyo, vunja ukimya,
zungumza naye! Si vibaya ukawa unazungumza na mpenzi wako juu ya mambo
yahusuyo uhusiano wenu. Muulize ni mambo gani ukimfanyia anasikia
furaha, akikuambia na mambo hayo yakawa ndani ya uwezo wako, jitahidi
kumtimizia.
5.Muulize, anachukizwa na mambo gani, akikuambia basi jiepushe nayo. Hata asipokuambia, ukimchunguza utayabaini tu.
Hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo ukiyazingatia yanaweza kukusaidia
katika kumfunga ‘spidi gavana’ kimtindo mpenzi wako ili asikusaliti.
Kama itatokea akakusaliti licha ya kumfanyia yote hayo, huyo siyo mtu wa
kuendelea kuwa naye.
No comments:
Post a Comment