NIMEKUWA
nikipata malalamiko mengi kutoka kwa baadhi ya wasomaji wangu
wakielezea jinsi wanavyosumbuliwa na wanaume, wengine wakidai wanataka
kuwaoa, wengine wakieleza wazi kuwa wanataka kufanya nao mapenzi tu tena
kwa ahadi ya malipo manono.
Kimsingi
hili ni tatizo sugu ambalo linaepukika lakini kuna ugumu kidogo katika
kuliepuka moja kwa moja. Mitaani tunakoishi wapo wanaume ambao wasione
msichana mrembo akipita, lazima wataanza kumsumbua kwa kumuita na
wengine kufikia hatua ya kuwashika sehemu zao nyeti bila ridhaa yao.
Mbaya
zaidi ni kwamba wanaume hao hufanya hivyo hata kwa wanawake ambao ni
wake za watu au wenye wapenzi wao. Tabia hii huwakera sana baadhi ya
wanawake hasa wale wanaojiheshimu na kuziheshimu ndoa na uhusiano wao.
Hata
hivyo, kuwaepuka wanaume wakware wakati mwingine huwa ngumu kwa kuwa
wengi wao hawana akili timamu, muda mwingi wao huwaza kufanya ngono tena
na kila mtu watakayemuona bila kufikiria madhara wanayoweza kuyapata
baadaye.
Niseme tu kwamba, wanaume wa aina hii wapo wengi tu huko mtaani ila kwa mwanamke anayeiheshimu ndoa yake au uhusiano wake na akaweka nia ya kuwaepuka, inawezekana!
Niseme tu kwamba, wanaume wa aina hii wapo wengi tu huko mtaani ila kwa mwanamke anayeiheshimu ndoa yake au uhusiano wake na akaweka nia ya kuwaepuka, inawezekana!
Niseme tu kwamba, wanaume
siku hizi wametawaliwa na tamaa zisizokuwa na msingi. Ukitaka wakusumbue
watakusumbua kweli na wakati mwingine wanaweza kukushawishi ukamsaliti
mpenzio wako.
Kikubwa ni mwanamke kuwa na msimamo. Kutokukubali kugeuzwa kiti cha daladala kwamba kila mtu anaweza kumchezea.
Lakini mbali na hilo, unajiwekea mazingira ya kuwafanya wanaume wakuheshimu na kugwaya hata kukutamkia maneno ya kijinga.
Lakini mbali na hilo, unajiwekea mazingira ya kuwafanya wanaume wakuheshimu na kugwaya hata kukutamkia maneno ya kijinga.
Vaa
kiheshima, acha utani wa kijingajinga na wanaume na hakikisha unakuwa
na tabia ambazo zitawafanya wanaume wakware wajue kwamba wewe ni mtu
mwenye ndoa yako usiyetaka kuutia doa uhusiano wako.
Hata hivyo, huko
mtaani unakopita unaweza kukutana na mwanaume anayejua fika wewe ni mtu
ulie kwenye uhusiano wako lakini anakusumbua kila siku huku
akikushawishi kwa njia mbalimbali.
Huyu hutakiwi kumchekea na
kumpuuzia, una kitu cha ziada unachotakiwa kukifanya. Nasema hivyo kwa
kuwa kuna wanaume vinga’nganizi. Unampa maneno makali ili akukome lakini
bado anaendelea kukusumbua.
Inapofikia hatua hiyo jaribu kumshirikisha mpenzi wako au mumeo.
Hiyo itasaidia sana kwani mumeo anaweza kuchukua hatua zinazostahili dhidi yake na hatimaye kuweza kupunguza kasi ya usumbufu huo. Kamwe usithubutu kukaa kimya.
Mbaya zaidi ni kwamba unaweza kukuta shemeji yako ambaye ni rafiki wa karibu wa mpenzi wako ama mwanaume anayemfahamu vilivyo mumeo akakutongoza. Huyu ni hatari sana na wala usisubiri akutongoze mara mbili. Siku ya kwanza tu atakayokutamkia maneno yake ya kipuuzi, kwanza geuka mbogo, mkaripie kwa ukali kisha mpe taarifa mpenzi wako.

Baada ya hapo, mwanaume huyo hutakiwi kumheshimu, mchukukulie
kama mjinga mjinga fulani. Nasema hivyo kwa kuwa mwanaume wa dizaini
hiyo akikutokea kisha ukawa unamchekea ipo siku anaweza kukulazimisha
kufanya naye mapenzi.
CREDIT: GLP
No comments:
Post a Comment