UHUSIANO
wenye amani na masikilizano ndiyo kitu ambacho kila mmoja wetu
anakihitaji na ikiwa hivyo unaweza ukajikuta unanawiri tu!
Wakati
mwingine unaweza hata kujikuta hujala chochote lakini ukajihisi
umeshiba eti kwa sababu tu umemuona mpenzio au kuwa naye karibu tu,
yaani yeye kwako ndiyo mambo yote, yeye ndiyo kila kitu kwenye maisha
yako! Huo ndiyo utamu wa maisha!
Naamini kabisa wapo ambao wako
katika aina hiyo ya mapenzi na hao wanatakiwa kumshukuru Mungu kwa
kuwaweka kwenye mazingira hayo.
Lakini sasa wakati wengine wakiishi
kwa raha katika maisha yao ya kimapenzi, wapo wengine wanaoishi na
wapenzi wao huku mioyo yao ikiwa imesinyaa, yaani hawana furaha kabisa!
Kwao
kila siku ni karaha na vituko vya makusudi kutoka kwa wapenzi wao licha
ya kwamba wanawapenda sana na kuonesha mapenzi yao yote.
Cha ajabu
sasa, licha ya baadhi ya watu kutokuwa na furaha katika maisha yao ya
kimapenzi eti wanahisi njia sahihi ni kuvumilia huku wakiamini siku moja
mambo yatabadilika.
Jamani, huenda nikawa na msimamo tofauti kidogo kwani mimi naamini mapenzi ya kweli ni pamoja na kumsikiliza mwenzio na kuheshimu hisia zake, hasa kwenye mambo yanayofaa.
Jamani, huenda nikawa na msimamo tofauti kidogo kwani mimi naamini mapenzi ya kweli ni pamoja na kumsikiliza mwenzio na kuheshimu hisia zake, hasa kwenye mambo yanayofaa.
Tofauti na hapo,
tabia ya kutokuwa msikivu, kutojali na kutokuwa mwepesi kubadilika ni
dalili tosha ya kutokuwepo kwa upendo wa dhati. Mapenzi, nijuavyo mimi
ni kupenda,
kupendwa, kusikilizana, kupatilizwa na kuheshimiana na si
kinyume chake!
Wakati mwingine unaweza kujikuta katika wakati mgumu
wa kuamua hatima ya uhusiano wako na mpenzio kwa kuwa unahisi unampenda
sana na kwamba hauko tayari kumkosa.
Ukweli ni kwamba, hata kama
huyo uliyenaye unampenda vipi lakini kama anaonesha kubadilika na
kutokupa ile furaha uliyotarajia, huna sababu ya kumng’ang’ania. Muache
aende zake kwani huenda kuendelea kuwa naye ndiyo kuyafupisha maisha
yako.
Inawezekana kuna mambo mazuri ambayo amekuwa akikufanyia huko
nyuma kiasi kwamba ukikumbuka unasita kufanya maamuzi ya kumtosa.
Sikiliza nikuambie kitu, unapokutana na hali hiyo elewa ni shetani
ambaye anataka kukufanya uendelee kuwa kwenye utumwa wa mapenzi.
Pata
ujasiri, yaliyopita katika uhusiano wako, yafanye kuwa historia kisha
fanya uamuzi sahihi. Uamuzi sahihi ni upi? Sidhani kama hapa panahitaji
darasa zito.
Uamuzi wa kwanza ni kukubali kuendelea kuwa kwenye uhusiano huo. Utaamua hivyo kama utaona kwamba uko tayari mapenzi yakuue lakini siyo kumuacha huyo uliyetokea kumpenda. Ila kumbuka wanaochukua uamuzi huu ni malimbukeni wasiyoyathamini maisha yao.

Uamuzi mwingine ambao naona ni sahihi ni ule wa kumuacha aende kisha wewe uyaache maisha yako yaendelee kuwepo.
Amini bila kuwa naye bado maisha yako yanaweza kuendelea kuwa ya furaha na wala huwezi kujuta. Utajutaje wakati alikuwa akikunyima furaha uliyoitarajia?
Amini bila kuwa naye bado maisha yako yanaweza kuendelea kuwa ya furaha na wala huwezi kujuta. Utajutaje wakati alikuwa akikunyima furaha uliyoitarajia?
No comments:
Post a Comment