Thursday, April 21, 2011

Mwanzo mbaya hutengeneza ndoa mbaya


MSINGI wa kuanguka kwa ndoa nyingi ni pale upande mmoja au pande zote zinaposhindwa kutimiza kile ambacho kinawapasa kufanya.

Kwa mfano yawezekana uko kwenye ndoa, ni kweli wewe ni mwanamume mwenye uwezo wa fedha, wengine wanawanunulia magari au kuwafanyia mambo mazuri wake zao.

Hata kwa wanawake pia, wapo ambao wamekuwa wakiwafanyia yaliyo mazuri waume zao hasa kwa kuwapa fedha na kadhalika, lakini wanashindwa kufahamu kuwa suala la kula vizuri au fedha sicho hasa muhimu kwa wanandoa.

La muhimu katika ndoa ni kuangalia pande zote, kwa mfano kama ni kweli uko sawa kwenye suala la fedha, unapaswa kuangalia pia katika suala la mahusiano na mahaba kwa ujumla, je, kama mwanamume, una uwezo wa kushughulika kama ambavyo mwanamume anapaswa.

Tafiti zinaonyesha kuwa katika siku za karibuni kumekuwa na wanaume wengi wenye kusumbuliwa na tatizo la nguvu za kijinsia... wengine ninapozungumzia suala hili, huwa wanaona kama nafanya masihara, lakini ukweli ni kwamba mwanamke anamhitaji mwanamume lijali, aliyekomaa, eeeh kiasi kwamba hata akiwa mbali anasema yaani yule mwanamum,e we acha bwana, sijawahi kuona.

Kwa kawaida inapaswa ukitoka katika chumba cha mahaba na mwanamke hadi akitema mate yaangukie kifuani sio chini. Eeeh akitema mate puu!!! Yaangukie kifuanitiii!!! Hapo ni sawa kabisa. Hizo ndizo nguvu zimpasazo mwanamume kuwa nazo.
Lakini zaidi ya yote, haitii raha hata kidogo, kuna watu kama namna ya kula kila siku ni kifo cha mende. tena wengine hawajishughulishi katika mahaba wengine wanasema aaah kama tayari niambie nataka kuwahi.

Vitu kama hivi kwa ujumla vinakinaisha mahusiano. Ni jambo la msingi sana katika maisha ya wanandoa kupenda kujifunza vitu vipya, kupenda kuangalia na kufahamu mwenzangu anapenda nini na nimfanyie nini.

Si vizuri kufanya kwa kujipendelea, kama ilivyo kwa wanaume walio wengi. Juzi nilikuwa nazungumza na kijana wa kabila fulani, ndiyo kwanza kaingia mjini kutokea kijijini, akawa ananiambia aaah mimi sitakaa nioe Dar es Salaam.
Nikamuuliza kwa nini akajibu kwamba wasichana wengi wa Dar es Salaam wana manjonjo eti mwanamke tikisika aaah mbaya kabisa.

Baada ya kumfuatilia kwa makini, kumbe aliingizwa mjini na baa medi fulani, alimfanyia mikogo na miondoko hadi alikoma mwenyewe wizi mtupu. Akawa anafikiri anamfurahisha, lakini kumbe kwa staili ya kabila la yule kijana, hakufurahi hata kidogo, zaidi ni kwamba kuanzia siku hiyo alimchukia.

Ni kwamba kuna baadhi ya makabila yanamzuia mwanamke kucheza wala kufanya chochote, wala kutumia mikono yake wala ulimi na kadhalika. Anapaswa kutulia tu, kama kuku kachinjwa.
Nisingependa kulitaja hilo kabila, ambalo huenda likawa ndilo pekee Tanzania kwa kuendeleza mila na utamaduni. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, wakati mwingine kabla ya kuibuka na manjonjo, muulize mwenzi wako ungependa umfanyie nini.

Unaweza kufanya kitu ukafikiri unatengeneza, kumbe unaharibu.
Ambacho nataka kifahamike ni kuwa, ni jambo la msingi kwa wanandoa kupenda kuwa na mazungumzo. Eeh hata nyumbani, utakuta mara nyingi wanawake wanapika vitu kwa mazoea, kwamba aaah mume wangu huwa anapenda wali au ugali. Lakini ni vizuri wakati fulani kumuuliza unaonaje nikakupikia tambi na kadhalika

Wiki iliyopita katika kuzungumza na watu mbalimbali walipenda kufahamu siri muhimu ya kumjua mtu kama ni mwaminifu kweli au la.

Unaweza kutaka kujua hili kama tayari mmeshaoana au hata bado. Ziko njia nyingi, ambazo binafsi naziona si nzuri. Iliyo nzuri na ambayo humkwazi mtu ni kwa wewe mwenyewe kufanya jitihada zako taratibu na kwa siri bila yeyote kufahamu.

Ziko njia kwa mfano kuangalia simu ya mwenzi wako ambayo kwa ujumla si nzuri, kwa sababu tayari akishajua kwamba huwa unaangalia, atamwambia huyo mwenzi wake kwamba asiwe anaitumia au asithubutu kupiga wala kutuma ujumbe, hadi yeye aanze.
Kimsingi kuna njia nyingi za kuujua ukweli, lakini leo naomba nitangaze kwako njia moja nzuri na ya kipelelezi. Naamini tangu umeanza kusoma magazeti, kusikiliza redio na hata kuangalia TV, hujawahi kuona hili nitakaloliongelea.
Licha ya kutumia njia zote, iwe ni kuwa karibu na rafiki zake na kadhalika, ambao kwa bahati mbaya wengine hawawezi kuwa na maelezo sahihi ya mtu husika. Ni suala la msingi wewe mwenyewe kufanya kile ambacho unaamini kwamba kitakusaidia.

Mara kadhaa nimekuwa nikizungumza kwamba wakati mwingine kama unataka kumjua mtu ambaye unataka kuoana naye, ni vizuri kuwa karibu na rafiki zake, ni sawa lakini kuna watu wengine wana siri kubwa.

Ukitaka kujua mtu kama ana siri kubwa au la, ni wepesi au ugumu wa kukupeleka nyumbani kwake anakoishi.
Mtu yeyote ambaye ni mgumu kukupeleka kwake, jua huyo ni mwenye siri kubwa na kwa kiasi fulani ni vigumu kumjua, labda kama ataamua kufanya hivyo yeye mwenyewe.

Kitaalam hata hivyo, kama mtu humuamini, si vizuri kumpeleka nyumbani kwako. Aidha katika nyakati hizi, acha kabisa tabia ya kumuonyesha mtu kwenye nyumba ambayo unaishi. Uwe makini na watu kwa sababu tumezungukwa na watu wengi wabaya.

No comments: