Mwanamke Anapenda Kupendwa! Mara Nyingi Wanawake Ndiyo Hasa Huwa Na
Mapenzi Ya Dhati Zaidi Kuliko Wanaume. Mwanamke Anapoamua Kuwa Na Mpenzi
Wake, Humpenda Kwa Moyo Wake Wote, Hivyo Hupenda Kuwa Salama Katika
Penzi La Dhati Kwako. Anapenda Uhuru, Anapenda Kujisikia Wazi Kwako
Mahali Popote.
Mwanamke Anajisikia Vibaya Sana
Anapokuwa Hana Uhuru Hata Wa Kukushika Mkono Mnakuwa Barabarani Pamoja.
Anapenda Penzi La Uwazi! Maana Mwingine Utakuta Akikutana Na Rafiki
Yake, Badala Ya Kumtambulisha Vizuri Kama Mpenzi Wake, Anaanza Kupatwa
Na Kigugumizi. Utamsikia Akisema: “Ah! Huyu Ni Rafiki Yangu Bwana,
Anaitwa Latipha....”Hili Ni Kosa Kubwa Linalofanywa Na Wanaume Wengi
Bila Kujua Ni Kosa. Mwanamke Anakosa Amani Ya Moyo Kutokana Na
Unavyomtafsirisha Mbele Ya Rafiki Zako. Anahisi Hayupo Salama. Lazima
Atajiuliza Maswali, Kwanini
Hataki Kunitambulisha? Kwanini Anashindwa
Kusema Mimi Ni Mpenzi Wake? Sifananii? Sina Mvuto Au Nina Tatizo Gani?
Hayo Yanaweza Kuwa Maswali Yatakayomuumiza Sana Kichwa Mpenzi Wako,
Ambaye Si Ajabu Akafanya Maamuzi Ambayo Hutayapenda.
Kidonda Hiki Hubaki
Moyoni Mwa Mwanamke, Huwa Vigumu Sana Kuonyesha Wazi Kwamba Amechukia
Kutokana Na Uliyomfanyia, Lakini Atabaki Akiugulia Moyoni Mwake Kwa
Uchungu. Hata Hivyo, Kinachokuja Akilini Mwake Ni Kutafuta Mwanaume
Mwingine Ambaye Atakuwa Wazi Kwake Ili Aweze Kufurahia Mapenzi Badala Ya
Kuendelea Kuumia Moyoni Mwake.
Ni Dhahiri Kwamba Uamuzi Huu
Hautaufurahia Hakika. 1. UNAVYOJALI... Mwanamke Anapenda Awe Wa Pekee
Kwako, Umsikilize, Umjali Na Umpe Kipaumbele Katika Kila Unachokifanya .
Wanawake Wengi Wanapenda Kudekezwa, Lakini Hawapendi Kuweka Hilo Wazi
Kwa Mwanaume Wake. Kwa Kumtazama Tu Utagundua Mpenzi Wako Anahitaji Nini
Zaidi Kwako! Wakati Mwingine Anaweza Kukupa Mitihani Ili Kupima
Kiwango Cha Penzi Lako.
Anaweza Kukuambia Anaumwa Au Anauguliwa Na Mtu
Wake Wa Karibu, Lengo Ni Kuangalia Ni Jinsi Gani Unakuwa Makini
Anapokuwa Na Matatizo. Vile Utakavyochukulia Tatizo Lake Kwa Ukaribu,
Uchungu Na Kuona Kama Lako, Ndivyo Utakavyomfanya Aone Thamani La Penzi
Lako Kwake, Ikiwa Vinginevyo Basi Humuacha Na Machungu Moyoni, Huku
Akijutia Kuwa Na Mpenzi Wa Aina Yako. Hii Ni Siri Ambayo Si Rahisi
Mwanamke Wako Akueleze Moja Kwa Moja. Atatumia Lugha Ya Ishara Kuonesha
Jinsi Ambavyo Anahitaji Kuwa Wa Pekee Kwako. 2. JIFUNZE SIRI HIZO.....
Hapa Ndipo Mwanaume Mwerevu Anatakiwa Kuwa Makini, Ni Lazima Ufahamu
Siri Zilizopo Moyoni Mwa Mpenzi Wako.
Jifunze Kusoma Hisia Za Mpenzi
Wako Kwa Nje, Kabla Ya Kufanya Kitu, Fikiria Mara Mbili, Lakini Baada Ya
Kufanya, Msome Kupitia Uso Wake. Analifurahia Au Umemchukiza? Ni
Vizuri Kugundua Hilo Ili Uweze Kufunga Hisia Za Kumfanya Aanze Kufikiria
Kukusaliti. Hata Mnapokuwa Faragha Ni Vizuri Kuwa Makini Na Kila
Unachokifanya! Chunguza Kama Anafurahia Penzi Lako Na Manjonjo Yote
Unayomfanyia. Kumbuka Kwamba Ni Vigumu Sana Mwanamke Kukueleza Moja Kwa
Moja Kwamba Hujamfurahisha Au Kuna Kitu Umekikosea, Hii Husababishwa Na
Hofu Ya Kuogopa Kukufanya Ujisikie Vibaya. Kwa Maneno Mengi WEWE
Mwanaume Ndiye Mwenye Kazi Ya Kuangalia Mwanamke Wako Anapenda Nini Na
Nini
Hapendi Ili Uweze Kuwa MWANAUME Wake Bora, Maana Hata Hisia Zake Za
Ndani Utakuwa Unazifahamu. Ni Rahisi Sana, Soma Kupitia Macho Yake Kila
Unachomfanyia, Utaujua Ukweli. Unajua Hata Ukimwita Kwa Jina Ambalo
Hana Msisimko Nalo Lakini Ukiwa Unamtazama Usoni Ni Rahisi Sana Kugundua
Kitu Fulani, Kama Hajakipenda Utaona Kwenye Macho Na Akikipenda Pia
Utaona.
Unapokuwa Naye Faragha, Tumia Uwezo Wako Wote, Lakini Kumbuka
Kwamba Si Kila Utakachokifanya Utamfurahisha. Hii Inamaanisha Kwamba,
Baada Ya Kumchunguza Jinsi Anavyosisimka, Utaweza Kugundua Wapi Kuna
Msisimko Zaidi Kuliko Sehemu Nyingine. Hapo Sasa Unaweza Kuibuka
MSHINDI Maana Utakuwa Umeziweka Siri Zake Hadharani, Kwa Maneno Mengine
Kama Yeye Aliona Siri, Basi Umeweza Kuzigundua Na Angalau Umeanza
Kuzifanyia Kazi. Nawapenda Sana Rafiki Zangu, Ndio Maana Nawapeni Mambo
Mazuri Na Yenye Sifa Ili Msiweze Kusababisha Kitu
Kinaitwa..."UMENITENDA/ AMENITENDA" (KUTENDANA NI DHAMBI KUBWA SANA) NIWATAKIE SIKU NJEMA..
No comments:
Post a Comment