Sunday, August 3, 2014

Kuna umuhimu gani wa kuwa na mwenzi wa maisha?

HAPANA shaka mtakuwa wazima wa afya njema na mnaendelea na majukumu yenu ya kila siku kama kawaida. Kwa upande wangu mimi ni mzima wa afya njema kwa uwezo wa Maanani.

Nikukaribishe tena katika mada yetu ya leo baada ya wiki iliyopita kumaliza mada ya kutambua thamani ya mapenzi.
Kabla sijaanza rasmi, niwakumbushe kwamba kitabu changu cha Joseph Shaluwa…Lets Talk About Love kipo katika hatua za mwisho kabisa ya kuingia mitaani.

Ni kitabu chenye mada nyingi za mapenzi pamoja na Love Messages zenye ujumbe murua wa mapenzi kwa ajili ya kumtumia mpenzi wako. Si cha kukosa.

Sasa tuanze mada yetu…hivi umewahi kujiuliza kwanini tunakuwa na wenzi wa maisha? Kwanini mapenzi yakawepo? Kwanini wewe una mpenzi na ikitokea mkawa mmehitilafiana unakosa raha? Sina shaka kuwa katika hili, kila mmoja anaweza kuwa na fikra zake mwenyewe, lakini leo nitafafanua sababu za msingi zaidi zinazowafanya wapenzi kuwa pamoja na hatimaye kuishi katika ndoa.

Lakini kabla ya kufika mbali zaidi hebu jiulize swali moja, mapenzi humaanisha nini hasa? Kimsingi mapenzi ni hisia za watu wawili ambazo hukutana pamoja zikimaanisha upendo wa dhati. Pendo hukamilika ikiwa wawili hao kwa wakati mmoja wakahisi hisia hizo, ingawa wakati mwingine mmoja ndiyo huwa wa kwanza kuanza kuhisi hisia hizo.

Wakati mwingine inawezekana mkajikuta mmependana tangu siku ya kwanza tu mlipokutana, lakini wengine huchukua muda mrefu kidogo kabla hisia hizo hazijachukua nafasi.

Wengine hutumia nafasi hii vibaya, baadhi yao huamini kuwa ngono ndiyo mapenzi yenyewe, jambo ambalo halina ukweli. Hebu fuatilia vipengele vifuatavyo kwa makini bila shaka kuna kitu utajifunza!

KUSAIDIANA MAWAZO
Hili ni jambo la msingi zaidi katika uhusiano, mwanaume kama mwanaume, kwa uwezo wake peke yake, hata kama ana uwezo mkubwa kifedha, siyo rahisi kutimiza mipango yake ya kimaendeleo kwa uwezo wa akili yake peke yake.

Huu ni ukweli ambao wanaume wengi huukwepa kwa kuhofia kale kamsemo ka ‘tulichuma pamoja’, kimsingi unapokuwa katika muunganiko hasa kama mwenzi wako ana hekima chanya, ni wazi kuwa kutakuwa na kitu kinachoongezeka katika maisha yako. Fikra za kuwa mwanamke ni mtu wa kuzaa na kuangalia familia pekee, ni fikra za kizamani zisizo na mantiki.

Waswahili walinena ‘wawili ni wawili’, msemo huu una maana kubwa tena yenye msingi katika maisha yetu ya kila siku. Unapoamua kuingia katika ndoa, urafiki au uchumba ni wazi kuwa utakuwa umeshajiingiza katika ulimwengu wa wawili! Hii ina maana kuwa hata katika mambo yahusuyo maisha yako binafsi, siyo ajabu mwenza wako, akapinga au kukusapoti kulingana na maono yake juu ya jambo husika.

Fahamu kuwa, mwenza wako ana haki ya kutaka kujua kila utarajiacho kukifanya na anaweza kukupinga au kuhitaji pointi za kutosha za wewe kutaka kufanya jambo hilo. Heshimu mchango wa mawazo ya mwezako, bila kujali jinsia, cheo au elimu yake, ukishaamua kuwa naye, mmekuwa kitu kimoja. Hii ni kati ya sababu za msingi sana za kuwa na mwenzi wa maisha.

VIPI KUHUSU KUKUTANA KIMWILI?
Mapenzi ni kitu kingine na ngono ni kitu kingine, ingawa baadhi ya watu hufikiria kuwa ngono ni sehemu ya uhusiano, jambo ambalo sio la kweli hata kidogo. Kimsingi ngono huja baada ya tamaa kuingia kati ya hao wawili wanaopendana!

Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa, ukawa na tamaa ya kufanya ngono na mtu hata kama huna mapenzi katika moyo wako. Kimsingi suala la kufanya ngono sio kithibitisho cha kuonyesha mapenzi ya dhati.

Baadhi ya walio katika uhusiano, hudanyanywa na kipengele hiki. Utakuta msichana anaambiwa na boyfriend wake kuwa, ili aonyeshe kuwa anampenda basi lazima akubali kufanya naye ngono, hata hivyo baada ya kumaliza kufanya ngono, kuna uwezekano mkubwa wa penzi hilo kuyeyuka!

Kuwa na msimamo, usikubali kuuza utu wako kwa gharama ya kumpenda mtu! Hebu soma kipengele kinachofuata kwa makini ili uweze kujua ni muda gani hasa ufaao kukutana kimwili na mpenzi wako.

MUDA MUAFAKA KUKUTANA!
Kimsingi suala la kufanya mapenzi halina kanuni, hakuna muda maalum wa kuanza kufanya mapenzi na mpenzi wako. Ngono ni hisia tu, tena basi huwa bora zaidi kama hisia hizo zikaja kwa wakati mmoja kati yako na huyo unayempenda!

Wataalam wa Saikolojia ya Mapenzi, wanashauri wapenzi wasishiriki tendo hilo mpaka pale watapokuwa wamefahamiana kiasi cha kutosha, hasa kupima afya kwakuwa magonjwa ya zinaa na ukimwi yamezagaa. Pamoja na hayo, suala la ngono halikwepeki ikiwa mtaruhusu kukutana sehemu tulivu mkiwa wawili.

Jambo la msingi ni kutulia na kujipanga, msifanye ngono kama sehemu ya mapenzi. Tambua kuwa ngono ni kitu kingine na mapenzi ni kitu kingine, hata kama mtakuwa mmeamua kushiriki katika kitendo hicho, mfahamu kuwa mnasterehesha nafsi zenu na sio kuonyeshana mapenzi ya dhati.

Lakini pia kuna vitu vingi ambavyo mnaweza kuvifanya ili kuepuka kufanya ngono, kama ni kweli mnapendana, mnaweza kutumia muda wenu vizuri kwa ajili ya kupanga maisha yenu yajayo, kucheza ufukweni pamoja na hata kupigana mabusu. Kila kitu kinawezekana ikiwa mtakuwa makini na wenye mipaka. Kwa leo naishia hapa, hadi wiki ijayo kwa mwendelezo wa mada hii ambayo sina shaka itakuacha na mafunzo makubwa katika maisha yako ya kimapenzi.source ya mada hii>>>Muandishi Joseph shaluwa

MPE NAFASI MPENZI WAKO KWA WANAUME WANAOKUSUMBUA KINGONO

NIMEKUWA  nikipata malalamiko mengi kutoka kwa baadhi ya wasomaji wangu wakielezea jinsi wanavyosumbuliwa na wanaume, wengine wakidai wanataka kuwaoa, wengine wakieleza wazi kuwa wanataka kufanya nao mapenzi tu tena kwa ahadi ya malipo manono.
Kimsingi hili ni tatizo sugu ambalo linaepukika lakini kuna ugumu kidogo katika kuliepuka moja kwa moja. Mitaani tunakoishi wapo wanaume ambao wasione msichana mrembo akipita, lazima wataanza kumsumbua kwa kumuita na wengine kufikia hatua ya kuwashika sehemu zao nyeti bila ridhaa yao.
 
Mbaya zaidi ni kwamba wanaume hao hufanya hivyo hata kwa wanawake ambao ni wake za watu au wenye wapenzi wao. Tabia hii huwakera sana baadhi ya wanawake hasa wale wanaojiheshimu na kuziheshimu ndoa na uhusiano wao.
 
Hata hivyo, kuwaepuka wanaume wakware wakati mwingine huwa ngumu kwa kuwa wengi wao hawana akili timamu, muda mwingi wao huwaza kufanya ngono tena na kila mtu watakayemuona bila kufikiria madhara wanayoweza kuyapata baadaye. 
Niseme tu kwamba, wanaume wa aina hii wapo wengi tu huko mtaani ila kwa mwanamke anayeiheshimu ndoa yake au uhusiano wake na akaweka nia ya kuwaepuka, inawezekana!
 
Niseme tu kwamba, wanaume siku hizi wametawaliwa na tamaa zisizokuwa na msingi. Ukitaka wakusumbue watakusumbua kweli na wakati mwingine wanaweza kukushawishi ukamsaliti mpenzio wako.
 
Kikubwa ni mwanamke kuwa na msimamo. Kutokukubali kugeuzwa kiti cha daladala kwamba kila mtu anaweza kumchezea.
Lakini mbali na hilo, unajiwekea mazingira ya kuwafanya wanaume wakuheshimu na kugwaya hata kukutamkia maneno ya kijinga.
 
Vaa kiheshima, acha utani wa kijingajinga na wanaume na hakikisha unakuwa na tabia ambazo zitawafanya wanaume wakware wajue kwamba wewe ni mtu mwenye ndoa yako usiyetaka kuutia doa uhusiano wako.

UAMINIFU SILAHA YA KWELI KATIKA PENZI

NI furaha iliyoje kukutana tena katika safu yetu nzuri ya kuelimishana juu ya mapenzi? Sina shaka utakuwa mzima wa afya njema na upo tayari kupata kitu kipya. Nakukaribisha kwa moyo mkunjufu tuongeze maarifa.

Rafiki zangu, leo nazungumza juu ya jambo muhimu sana katika mapenzi; uaminifu. Huu ndiyo msingi wa uhusiano, ndoa na mapenzi. Ikiwa uhusiano utakosa uaminifu, ni wazi kwamba hautakuwa na umri mrefu.

Uaminifu ni jambo lenye mvutano mkubwa, ni mjadala usiokwisha tangu kuwepo kwa mapenzi. Ukweli ni kwamba uaminifu ndiyo kipimo cha kwanza cha kugundua kama penzi lako ni la kweli au moyo wako unakudanganya.

Hata hivyo upo ukweli ambao hauwezi kukwepwa! Uaminifu unawashinda wengi sana walio kwenye uhusiano. Watu wanashindwa kuwa waaminifu kabisa. Pamoja na yote hayo, zipo sababu ambazo zinaelezwa zinasababisha mwenzi kukosa uaminifu kwa mpenzi wake.
Hebu twende tukaone ni kwa nini watu wanakosa uaminifu.

KUKULIA KATIKA IMANI...
Hili ni la kwanza kabisa ambalo unapaswa kulifahamu rafiki yangu mpenzi, malezi ya kiimani! Neno uaminifu tukilinyambua tunapata maneno imani, amini na aminiana. Kwa msingi huo basi, ikiwa mpenzi wako hajakulia katika mazingira mazuri ya kiimani kulingana na taratibu za dini anayoiamini ni vigumu sana kuwa mwamnifu au kukuamini!Hii ina maana kwamba wakati unachagua mchumba ni vizuri kuangalia pia suala la imani ya dini yake.

Je, ni muumini kikamilifu katika imani yake? Maana katika imani za dini, kitu cha kwanza kabisa kufundishwa na kutiliwa mkazo ni uaminifu! Katika uaminifu huwezi kukuta uongo, usaliti, masengenyo na mengine mengi ambayo siyo mema.
Mwaminifu ana hofu, atapenda kuzungumza ukweli siku zote maana imani ya dini yake inamsuta.

Friday, September 6, 2013

UNAWEZA KUPENDA SANA ASIKUPENDE, FANYA UAMUZI SAHIHI SASA!

UHUSIANO  wenye amani na masikilizano ndiyo kitu ambacho kila mmoja wetu anakihitaji na ikiwa hivyo unaweza ukajikuta unanawiri tu!  
Wakati mwingine unaweza hata kujikuta hujala chochote lakini ukajihisi umeshiba eti kwa sababu tu umemuona mpenzio au kuwa naye karibu tu, yaani yeye kwako ndiyo mambo yote, yeye ndiyo kila kitu kwenye maisha yako! Huo ndiyo utamu wa maisha!
 
Naamini kabisa wapo ambao wako katika aina hiyo ya mapenzi na hao wanatakiwa kumshukuru Mungu kwa kuwaweka kwenye mazingira hayo.
 
Lakini sasa wakati wengine wakiishi kwa raha katika maisha yao ya kimapenzi, wapo wengine wanaoishi na wapenzi wao huku mioyo yao ikiwa imesinyaa, yaani hawana furaha kabisa!
 
Kwao kila siku ni karaha na vituko vya makusudi kutoka kwa wapenzi wao licha ya kwamba wanawapenda sana na kuonesha mapenzi yao yote.
 
Cha ajabu sasa, licha ya baadhi ya watu kutokuwa na furaha katika maisha yao ya kimapenzi eti wanahisi njia sahihi ni kuvumilia huku wakiamini siku moja mambo yatabadilika.
Jamani, huenda nikawa na msimamo tofauti kidogo kwani mimi naamini mapenzi ya kweli ni pamoja na kumsikiliza mwenzio na kuheshimu hisia zake, hasa kwenye mambo yanayofaa.  

Friday, August 30, 2013

Wivu chandandu ya mapenzi, lakini ikizidi huwa karaha

WOTE tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kutufikisha siku hii. Naungana na familia za wote waliopatwa na janga la ajali ya kuzama kwa meli wiki iliyopita. Mungu awape moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu, pia waliotangulia mbele ya haki mwenyezi Mungu awape mapokezi mema.
Kama kawaida tunaendelea mada nyingine jinsi unavyoweza kuudhibiti wivu wako. Hakuna asiyejua wivu ni nini hasa katika suala ya uhusiano. Kila kiumbe chenye akili timamu lazima kiwe katika hali hiyo.
Wivu wa mapenzi unamaanisha nini?
Wivu katika mapenzi unamaanisha mtu kumiliki mpenzi wake peke yake pasipo kuingiliwa na mwingine, kwa maana nyingine kuonyesha unampenda na kumjali ila ukizidi unakuwa sumu.
Kiumbe kisicho na wivu ni sawa na mwili bila roho ambacho lazima kitakuwa ni mfu.

Lakini kwa kiumbe kinachovuta pumzi lazima kiwe katika hali hiyo na kama huna huku bado unavuta pumzi basi hujui nini maana ya kupenda. Lakini kwa yeyote anayeijua thamani ya kupenda lazima atakuwa anajua maana ya wivu.

Wivu katika mapenzi ndiyo chachandu kwa mtu kujua kweli anapendwa. Huwezi kuwa na mke au mume akichelewa au kusimama mazingira yasiyo eleweka ukae kimya, ujue lazima kuna walakini akilini mwako.

Lakini leo nataka kuzungumzia wivu uliovuka mipaka ambao huwa kero kwa wengine. Wapo wanaume au wanawake huwaonea wivu hata dada au kaka yako.

Katika suala hili napenda kulieleza kwa mapana kwa ajili ya kwenda pamoja ili tuweze kupunguza wivu ambao umekuwa kero kwa watu hata kufikia kuvunja uhusiano. Jambo hili niliwahi kulizungumza awali kuwa hakuna kiumbe anayewaza ngono kila, wakati ukiona hivyo ujue ana matatizo.

Wednesday, August 28, 2013

UMESHINDWA KUWA MWAMINIFU KWA MPENZI WAKO?

Hapa nazungumza na wale ambao wanatamani kuwa waaminifu kwa wapenzi wao. Yapo mambo mengi, lakini hapa ninajitahidi kueleza yale ya muhimu zaidi. Wiki iliyopita niliishia kwenye kipengele cha mitandao ya kijamii, kwa kuwa sikukimaliza, tutaendelea hapo.
MITANDAO YA KIJAMII
Utafiti usio rasmi unaonesha kwamba, pamoja na kwamba mitandao ya kijamii imesaidia kwa kiasi kikubwa sana kurahisisha upatikanaji wa taarifa, kuendesha mijadala na kukuza ufahamu wa mambo mengi, suala la mapenzi limetajwa!

Utakutana na mtu Facebook (mfano), mmekuwa marafiki, lakini siku ya siku anaanzisha mambo ya mapenzi. Kwa sababu umeshakuwa naye karibu kwa muda mrefu, umekuwa wazi kwake ni rahisi kuanguka!
Hisia za mapenzi wakati mwingine hudanganya. Ngoja niwaambie ukweli, unapokuwa unawasiliana sana na mtu wa jinsi tofauti na yako, hisia za mapenzi huwa kali sana, kiasi kwamba ukiambiwa tu unapendwa, ni rahisi kuingia mkenge!

Kwenye mitandao ya kijamii kwa mfano Facebook, BBM, Twitter na mingineyo maarufu kuna utamaduni wa kuweka picha. Wakati mwingine picha hudanganya...kwa haraka haraka mtu eti anasema amekupenda. Hakuna lolote zaidi ya kuwaza ngono tu!
Huo ndiyo ukweli. Tatizo ni kwamba, huwezi kujua kama kuna hatari hiyo mbele yako. Unao marafiki wengi, mnataniana kila wakati, siku akilianzisha, inakuwa ngumu kuchomoka. Hata hivyo, kuna mambo madogo sana ukiyafanya yatasaidia kukutoa kwenye mtego.

Njia 5 za kupunguza tumbo kirahisi

WADADA au WAMAWAKE wengi wanatamani kuwa na matumbo madogo, lakini wengi hushindwa kufikia ndoto hiyo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za uzazi na kupenda chakula. Makala hii inaangalia njia rahisi ya kupunguza tumbo.

1. Uangalifu katika kula
Epuka chakula chenye wanga, mafuta mengi na sukari. Badala yake unaweza kula matunda na mboga za majani. Vile vile samaki wa baharini si wabaya kwani hawana mafuta mengi.

2. Namna ya kula
Usiache kula kwani jambo hilo litakunyima nguvu, unatakiwa kula milo mitatu mpaka minne lakini kwa kiasi kidogo. Unatakiwa kukaa zaidi ya saa tatu kabla ya kula mlo mwingine.

3. Mazoezi ya kawaida
Si lazima ufanye mazoezi makali kwa ajili ya kupunguza tumbo. Unaweza kufanya zoezi la kutembea badala ya kupanda basi, kama hufiki mbali sana. Kama unaweza kuogelea, unaweza kufanya hivyo mara kwa mara, hiyo pia itakusaidia.

4. Zoezi maalum
Kama unaweza kufanya zoezi la kulala chali na kukaa, 'abs exercise' unaweza kufanya kwa dakika chache kila siku. Hiyo itasaidia kukomaza misuli ya tumbo hivyo tumbo kutokulegea.

5. Kunywa maji
Maji yanasaidia mmeng'enyo wa chakula, hilo husaidia mtu kuwa na afya njema. Kwa kuwa mtu akiwa katika hatua za awali za kupunguza tumbo husikia njaa mara kwa mara, ni bora anywe maji badala ya kula.

Monday, August 26, 2013

USANII, UJANJA NA UTAPELI UNAVYOTUTIBULIA MAPENZI.

NDUGU zangu, tafsiri ya mapenzi kwa harakaharaka ni hisia ambazo zipo moyoni mwa mtu kwenda kwa mwingine, hisia hizi ili ziweze kuwa mapenzi ni lazima ziwe na ukweli na za dhati huku moyo ukiwa na nafasi kubwa katika hilo.
Pamoja na ukweli huo juu ya mapenzi lakini hivi sasa maana halisi ya mapenzi imepotoshwa, imebadilishwa na kuwa nyingine. Mapenzi ya siku hizi yamejaa ulaghai mtupu, hayana ukweli, kila siku ni maumivu juu ya maumivu. Kwa nini watu wanaharibu maana halisi ya mapenzi?
 

Kuna matatizo mengi ambayo yanaweza kutokea ikiwa utakosa uaminifu kwa mpenzi wako, wakati mwingine matatizo hayo huweza kumlenga mwenzi wako moja kwa moja bila kukusumbua wewe lakini mwisho wa siku wewe utakuja kuwa na matatizo zaidi ya hayo unayoyafanya nyuma ya pazia hivi sasa.
 

Unaweza kujifanya mjanja sana kwa kuunganisha wapenzi zaidi ya kumi huko gizani ukiamini huonekani na hakuna matatizo yoyote ambayo unaweza kuyapata, kumbe unajidanganya maana kuna siku utakuja kuumbuka kwa kuonekana kwako huna uaminifu!
 

Hivi ni kwa nini maana halisi ya mapenzi hivi sasa imepotoshwa? Ni nani muanzilishi wa upotoshaji wa maana halisi ya mapenzi, utagunduaje kama mpenzi wako ni msaliti wa penzi lako. Haya na mengineyo utayapata katika mada hii, unachotakiwa kufanya ni kufuatana nami.

UTAPELI, UJANJA, USANII...
Wengine huwa ni tabia yao ya asili, siyo mkweli kuanzia malezi ya wazazi wake kwani hayasisitizi juu ya ukweli. Ameshazoea kufanya mambo kiujanja ujanja! Kwa mpenzi wa aina hii ni vigumu sana kudumu naye.
 

Ni mwepesi wa kutamka maneno ya mapenzi lakini ndani ya moyo wake kuna vitu viwili, kwanza anakutamani wewe na pesa zako na wakati huohuo anatamani kuwa na bwana mwingine kwa ajili ya kuongeza kitega uchumi, hili ni tatizo!
 

Mwanamke wa aina hii siyo vigumu kukuita majina mazuri ya kimapenzi lakini akiwa hamaanishi kutoka moyoni mwake kwamba anakupenda. Hawa wapo wengi lakini ni vigumu sana kuwagundua mapema. Hawa huharibu kabisa maana halisi ya mapenzi.
 

Ngoja nikuulize wewe unayemsaliti mpenzi wako, unavyomfanyia mwenzako hivyo unadhani yeye hana moyo? Hivi hujui kuwa mwenzako anakupenda kwa mapenzi yake yote na amekuchagua wewe uwe mwandani wake? Siku akijiua kwa sababu yako utakuwa katika hali gani? Hebu acha utapeli wako wa mapenzi haraka sana!
 

Kuwa muwazi na kama unadhani haupo tayari kuwa na mpenzi basi mwache huru atafute mwingine mwenye msimamo uendelee na mambo yako na kama ni kujiuza ujiuze vizuri lakini ukijua kuwa siku moja utakuja kuingia mahali pabaya. Achana na tamaa za muda mfupi ambazo mwisho wake ni mbaya.
 

Huyo mwanaume anayekudanganya leo, ujue kabisa kesho hayupo na wewe na atakuwa amekuachia virusi vyako vya kutosha! Kama umeamua kujitoa sadaka ni bora ukafa peke yako kuliko kumwangamiza na mwenzako ambaye hana hatia zaidi ya penzi lake la dhati kwako.

USHAWISHI...
Hili ni tatizo lingine linalochochea kuharibu maana ya mapenzi, ushawishi ni sumu nyingine katika hili. Hapa nitazungumzia pande mbili, ya kwanza ni ya mshawishi na mshawishiwa! Naweza kusema wote wana makosa maana anayeshawishi hutumia kila njia kumpata anayemhitaji lakini wakati huohuo anayeshawishiwa kukubali wakati akijua ana mpenzi ni kosa kubwa sana.
 

Wanaume wengi watu wazima tena wenye familia zao hivi sasa ndiyo wanaoongoza kutafuta dogodogo wakidai kuwa damu zao zinachemka! Hutumia fedha, magari na kila aina ya vishawishi ili waweze kuwanasa wasichana hao wadogo wakitafuta penzi. Sijui wanaume wa aina hii wanatafuta nini kwa hao mabinti?

Itaendelea wiki ijayo.

Je unataka kupata mke/mume wa kweli? Fuata njia hizi!


JITAMBUE
Kwanza wewe kama mwanamke/mwanaume mwenyewe unatakiwa ujifahamu na kufahamu vigezo vya mpenzi unayemhitaji katika maisha yako.
Wanawake/wanaume wengi hawajui wanahitaji wapenzi wa aina gani, hivyo wanajikuta kama watu wanaoingia sokoni bila kujua wanataka kununua nini? Ndiyo maana wengi wameangukia kwa matapeli wa mapenzi, wakachezewa na kuumizwa moyo bure.

SIFA ZA UMTAKAYE
Keti chini na kuorodhesha vigezo vya mwanaume/mwanamke unayemtaka. Baada ya hapo orodhesha tena kasoro za mwanaume/mwanamke unazoweza kuzivumilia na zile ambazo huwezi kuzivumilia kabisa. Hii inatokana na ukweli kwamba mwanadamu hajakamilika, ana upungufu wake.  

TUMIA MACHO
Anza kumsaka huyo mwanaume kwa kutumia milango ya fahamu. Cha kufanya hapa ni kuruhusu macho yawaone wanaume/wanawake na kuwatathmini kwa maumbile yao ya nje na kisha kupata majibu kutoka moyoni juu ya kuvutia kwao ambako hutambulika kwa moyo kuridhika na mwili kusisimka.

JENGA MAZOEA NAYE
Kuanzisha safari ya kuchunguza tabia za nje na za ndani kivitendo. Hapa suala la ukaribu baina ya mwanaume na mwanamke linahitajika. Msingi unaotajwa hapa ni kujenga mazoea ya kawaida yasiyokuwa na masuala ya kimapenzi na ngono. Kutambuana, dini, viwango vya elimu, kabila na makundi ya marafiki ni mambo ya kuzingatia.

Katika uchunguzi huu mwanamke/mwanaume anayetafuta mpenzi hana budi kupitia na kumlinganisha huyo aliyempata na vigezo alivyojiwekea. Zoezi hili liendane na kuweka alama ya pata kila anapobaini kuwa mwanaume/mwanamke anayemchunguza amepata moja ya vigezo vyake. Lakini pia aweke alama ya kosa kwa kila kasoro anayoivumilia na ile asiyoivumilia.

HAKIKI SIFA ZAKE
Jipe muda wa kutosha kati ya miezi sita na mwaka kumchunguza huyo mwanaume, kisha keti chini na anza kujumlisha alama za vigezo ulivyovijiwekea na jinsi mwanaume huyo alivyopata au kukosa.

Ikibainika uliyechagua amepata zaidi ya nusu ya alama ya vigezo vilivyowekwa, basi ujue kuwa anafaa. Kuhusu alama chache alizokosa unaweza kumsaidia kuzikamilisha pole pole mkiwa kwenye maisha ya ndoa.

Lakini angalizo kubwa kabisa ni kwamba mwanaume/mwanamke akionekana kuanguka katika kasoro zisizoweza kuvumilia kwa zaidi ya alama tatu. Yaani kwa mfano ni mlevi, mwizi, muongo, mbishi na katika hizo kashindwa 3, huyu hafai, ni vema akawekwa kando kwani huwezi kubeba kero 3 kwa pamoja katika maisha.

WEKA MALENGO
Lazima baada ya kuchunguzana kwa kina wapenzi watengeneze muongozo wa mapenzi yao. Wasiwe kama wanyama, lazima mipango ya wapi wametoka walipo na wanapokwenda waifahamu.
Hata hivyo, wataalamu wanasema lazima wapenzi wapime umakini wao kwa vitendo. Kama wamekubaliana kuoana, suala la mume kwenda kujitambulisha kwa wakwe na hatua ya kuiendea ndoa ionekane. Usiri usiwepo tena. Kila mmoja amuone mwenzake kama sehemu ya maisha yake na mara zote wasaidiane kwa ukaribu.

USHIRIKI WA NDUGU/MARAFIKI
Ni vema ndugu wakashirikishwa ili kuwapa nafasi na wao ya kuamua kama mapenzi hayo ni budi yakaendelea au yakasitishwa. Ni ukweli ulio wazi kwamba licha ya wengi kupuuza maamuzi ya ndugu kwa madai ya kuwa hawana nafasi kwa wapenda nao, lakini uchunguzi unaonesha kuwa wapenzi wengi huachana kutokana na sumu za ndugu hasa pale wanapokuwa wameonesha kutounga mkono uhusiano wa wanaotaka kuoana.

TENDO LA NDOA
Hatua hii ni ya kuweza kuzungumzia ufanyaji mapenzi, hapa nina maana kama wapenzi wamejizuia kwa muda mrefu na wanahisi kuchoka wanaweza kujadiliana kuhusu tendo la ndoa na kuamua kuwa pamoja huku wakizingatia suala la afya na uzazi salama.

NDOA
Kutimizwa kwa ahadi ya kuoana ni hatua ya tisa ambayo nayo si vema ikachukua muda mwingi kutekelezeka, kwani ucheleweshaji mwingi wa ndoa nao huvunja moyo na mara nyingine umewafanya wengi kutoaminiana.

UVUMILIVU
Kuamua kuwa mwili mmoja kwa kuvumilia na kuwa tayari kukabiliana na changamoto zote za maisha ukiwemo mkwamo na dhiki ambazo huchangia sana ndoa nyingi kuvunjika. Hapa pia ni wajibu wa wanandoa kuchukuliana udhaifu na kusaidiana.

Kuwa tayari kujifunza na kujali zaidi upendo kuliko hisia za mwili ambazo wakati mwingine hudanganya hivyo kumfanya mwanandoa asivutiwe na mwenzake.source ya mada hii>>>www.globalpublishers>>>Muandishi Joseph shaluwa

Wednesday, August 21, 2013

Kama unahitaji kudumu na mpenzi wako, soma hapa!


NAKUKARIBISHA kwa moyo mkunjufu kwenye safu yetu maalum kwa ajili ya kupeana ujuzi katika anga ya sanaa ya mapenzi. Ni imani yangu, umekuwa ukipata maarifa mapya kila siku kupitia hapa. Kaa tayari uvune kitu kipya leo.

Kwanza kabisa, napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wote ambao mmekuwa mkiwasiliana nami kwa njia ya simu na kunipongeza, kunikosoa na kuuliza maswali kuhusu mambo mbalimbali yanayowakabili katika uhusiano. Kufanya kwenu hivyo kunanipa moyo kwamba, ujumbe unawafikia vilivyo.

Sasa twende moja kwa moja kwenye mada yenyewe. Nazungumzia juu ya mambo ya kuzingatia kama unahitaji kudumu katika uhusiano ulionao. Hapa naomba nizungumze na wanawake zaidi. Nasema hivyo kwa sababu wao ndiyo wanaokumbana zaidi na matatizo ya kuachwa na wapenzi wao kuliko wanaume.

Ni sahihi kusema, wanawake ndiyo huumizwa zaidi katika mapenzi kuliko wanaume. Hii ni kutokana na sababu kubwa mbili; kwa kawaida wao ndiyo hufuatwa na kutongozwa na wanaume, lakini lingine ni kwamba, mara nyingi wanaume ndiyo hutoa uamuzi wa kuacha au kuachana.

Kwa sababu hizo, hakuna ubishi kuwa wanawake ndiyo welengwa wakubwa wa mada hii. Rafiki zangu, kuna mambo kadha wa kadha ambayo yanaweza kusababisha uhusiano kuwa butu na baadaye kuishia njiani.

TAMBUA THAMANI YAKO
Ili uweze kuwa bora ni lazima uanzie kwako, ujitambue kama mwanamke na thamani yako kwa mwanaume wako.  Ukiijua thamani yako, lazima utakuwa makini na kila kitu. Rafiki yangu, ninaposema thamani ninamaanisha kwanza kujiamini na kujipa nafasi ya kwanza.

Uamini kwamba wewe ni mwanamke mrembo na unayevutia. Imani hiyo ikishaingia, tayari utakuwa unajali mambo mengi ya msingi, ikiwemo usafi wako binafsi. Waswahili wanasema, mwanamke ni pambo la nyumba. Pambo haina maana ya ua, inamaanisha ule usafi wa kila kitu.

Kwamba nyumba bila mwanamke haiwezi kukamilika, wewe kama mwanamke unatakiwa kufahamu wewe ni kila kitu ndani ya nyumba. Umakini wako na kujitambua ndiyo vitu vitakavyokuweka katika nafasi nzuri ya kudumu katika uhusiano wako na baadaye kuingia kwenye ndoa.

TAMBUA THAMANI YAKE
Ukiijua thamani ya mwanaume kutoka ndani ya moyo wako ni wazi kwamba hata vipengele vifuatavyo hapa chini havitakuwa vigumu kwako kutekelezeka. Inakupasa ujue thamani ya mwanaume wako ipasavyo.

Hilo si tu kwa maneno, bali ni jambo ambalo linatakiwa kufanyika kwa ridhaa ya moyo wako. Ni rahisi zaidi jambo hili kufanyika ikiwa utakuwa na mapenzi ya dhati. Mpende kwa moyo wako wote na ujue kuwa maisha yako yanakamilishwa na uwepo wake.

Ndiyo! Yanakamilishwa na uwepo wake, maana una mategemeo ya kuingia katika ndoa naye. Hapo mtakuwa mwili mmoja na maisha ya kila mmoja yatamtegemea mwenzake.

MHESHIMU
Mwanaume anapenda sana kuheshimiwa na mpenzi wake. Mwanaume akigundua haheshimiwi au unafanya hivyo kwa kumridhisha tu na si kutoka moyoni, ni rahisi kukuacha.

Kama kichwa cha familia, lazima apewe nafasi ya kutoa uamuzi tangu mapema. Ikiwa utakuwa na majibu mabaya kwake, humheshimu ni wazi kwamba atakuacha mapema, maana utakuwa umepoteza sifa za kuwa mama wa familia.
Mada bado inaendelea, wiki ijayo usikose sehemu ya pili.

PENZI LAKO LIMECHUJA, UNAJUA CHANZO?

Ni wiki nyingine tulivu kabisa tunakutana kupitia safu hii maridhawa kabisa ambapo pamoja na mambo mengine tunazungumzia mada mbalimbali zinazohusu uhusiano wa kimapenzi.
 
Wiki hii nitazungumzia suala la penzi kuchuja. Ipo hali ya kujisahau baada ya wapenzi kuwa katika uhusiano kwa muda mrefu, haieleweki kama ni tabia ya mtu ama ni uhalisia wa mambo kwasababu ukweli ulio wazi ni kwamba, mwanzo wa uhusiano wengi hujitahidi kufanya mambo mengi ya kuwafurahisha wapenzi wetu lakini kadiri siku zinavyosogea, penzi huanza kuchuja.
Kama huamini katika hili, rudisha nyuma kumbukumbu zako kipindi kile ambacho ndio jamaa kaamua kukueleza wazi kwamba anakupenda halafu angalia na sasa hivi, utabaini kwamba kuna tofauti kubwa sana.
 
Huenda mlikuwa na desturi ya kununuliana zawadi kama maua, kadi, chokoleti tabia hiyo huenda ikawa imeyeyuka, hakuna kati yenu atakayekumbuka kitu hicho, ni wachache sana ambao wanakwenda na wakati ndiyo huendelea kuzingatia hayo.
 
Kuna wale ambao walikuwa na tabia ya kukutana kila mara kimapenzi ambapo kila mmoja alitaka kumuonesha mwenzie jinsi  alivyo fundi wa 'kuyarudi' ndani ya uwanja wa mapenzi lakini yale manjonjo huadimika kabisa.
 
Kawaida yenu ilikuwa kubadilisha hoteli kwa ajili ya chakula cha jioni lakini tabia hiyo hutoweka, labda kila wiki ilikuwa lazima muende 'out' mara tatu katika kumbi tofauti za starehe na kufurahia mapenzi yenu, hali hiyo itabaki historia tu.
 
Hivi hujawahi kusikia mtu anasema "Enzi zile naanza uhusiano na mpenzi wangu mapenzi yalikuwa moto moto, kila wiki ilikuwa lazima twende beach lakini, siku hizi nikigusia tu kwenda huko ni ugomvi."
 
Maneno kama haya huwa yananiuma sana hasa ninapogundua kwamba walio wengi wanakuwa na nguvu ya soda pale wanapoingia katika uhusiano lakini baada ya muda mambo hubadilika kabisa.
 
Sijajua ni kwasababu gani lakini kwa utafiti mdogo ambao nilioufanya kwa baadhi ya wanaume ni kwamba, wao wanapofanikiwa ‘kuona ndani tu’ hujenga kiburi fulani kwa wasichana wao huku wakiamini kwamba, hata wawe tofauti vipi hawawezi kuachwa!
Labda nijaribu kushauri kitu katika hili kwamba, kama uko kwenye uhusiano wa kimapenzi ama uko ndani ya ndoa, unatakiwa kufanya kila linalowezekana kulifanya penzi lenu lisichuje.
 
Wewe ndio unaweza kulifanya likaendelea kuonekana kuwa jipya kila siku ama kulifanya likachuja mithili ya nguo inayochuja rangi iliyotumbukiza katika ndoo ya maji ya moto.
 
 
Hatukatai kwamba, kuna mabadiliko ya kimaslahi, pengine mtu na mpenzi wake wameketi na kuona wanatumia pesa nyingi viwanja, kwahiyo wanaamua kupunguza au kuacha ili kujenga maisha bora ya baadae, si unajua tena mnapokuwa na malengo ya kimaisha zaidi?
 
Lakini ukweli unabaki palepale kwamba, penzi la dhati haliwezi kuchuja hata siku moja. Tujue wapo ambao wameishi miaka zaidi ya hamsini lakini penzi lao bado ni moto licha ya kuwepo kwa mabadiliko madogo ambayo hayakwepeki kutokana na umri.
 
 
Yapo mabadiliko mengi, lakini zaidi tujirekebishe, tukumbuke kwamba baadhi ya vitu tulivyokuwa navyo huko nyuma ndivyo viliwavutia wepenzi wetu na kukubali kuwa nasi kwa hiyo tukiacha tunakuwa tunawakatili.

Fedha, uzuri si kinga ya mapenzi, kuna kitu cha ziada


WAKATI akili yangu ikianza kupata ufahamu, nilikuwa natatizika na kuwaza kitu gani hasa katika mapenzi kinaweza kumfanya mtu atulie ndani ya penzi lake. Niliamini kuwa na fedha ndiyo dawa ya mtu kumtuliza mpenzi wake au kwa mwanamke kuwa mzuri na mwenye sifa zote, ndiyo dawa ya kumfanya mpenzi wako atulie.
Baada ya kukua na kuingia katika dunia ya ufahamu wenye mitihani mingi ya mapenzi, nimegundua kuna utofauti mkubwa katika vitu nilivyoviwaza.

Wakati nakua, nilikutana na matukio ambayo niliona kama ngamia kupita kwenye tundu la sindano, lakini baada ya kupevuka, nilipata majibu ya maswali yaliyonisumbua kipindi kile cha utoto.
Sikuamini mke wa tajiri kufanya mapenzi na muuza mchicha, mwanaume mwenye mke mzuri kutembea na changudoa au msichana wa kazi asiyejua kuvaa wala kuoga.
Baada ya kuingia katika kazi hii ya kukumbushana mambo ya mapenzi, nilipata maswali mawili ya watu wawili tofauti lakini yalikuwa na jibu moja.

Mmoja alilalamika ana mke, anamhudumia kila kitu ikiwemo familia yake lakini alichomlipa ni kutembea na mtu asiye na mbele wala nyuma. Mwingine alilalamika kuhusu mpenzi wake kutembea na mwanamke wa nyumba ya pili ambaye haufikii hata mguu wake kwa uzuri.
Kabla ya kulizungumzia hilo, nirudi kwao kuwaeleza kukosa uamini hakuangalii katembea na tajiri au mwanamke anayekushinda uzuri, kutoka nje ya uhusiano au ndoa ni kosa kwa vile penzi ni la watu walioridhiana au kuoana wakiwemo waliooa wake zaidi ya mmoja.

Leo nawajibu wote kuwa fedha au uzuri wa mtu havibebi ndoa au uhusiano. Nimekuwa muumini mzuri wa kuwaeleza penzi la kweli lipo vipi, mapenzi ni upendo wa dhati kutoka moyoni, kuwa tayari kujilinda na kujiheshimu bila kujali una fedha au ni mwanamke mzuri.
Mapenzi ni mbegu inayohitaji udongo wenye rutuba ya upendo ili mbegu hiyo imee. Siku zote mwenye mapenzi ya kweli humuangalia mtu, si kitu.

Tajiri na fedha zake asipopendwa huwa katika mateso na kukonda wakati ana kila kitu. Penzi la kweli halinunuliwi kwa gharama yoyote.
Tabia ya asili huwa sawa na moto unaowaka kwenye pamba, ukitoa moshi ujue hakuna kilicho salama. Wapo watu wasiokuwa na mapenzi ya dhati, utakuta mtu anajifanya anakupenda ukiwa naye lakini mkiachana hana habari na wewe, hata kama mnakaa nyumba moja na kulala kitanda kimoja.
Mtu anapoamua kutoka nje ya ndoa wakati ndani ana mke mzuri au mume wa ukweli anayempa kila kitu, kuna mawili:
Mosi:
Huenda mwanamke aliyenaye alimtamani kutokana na sura na umbile lake na hakumpenda kwa dhati. Matokeo yake baada ya kumchoka, mwanamke huonekana hafai na hukaa naye kimazoea.
Upande wa mwanamke, naye huenda amekwenda kwa mwanaume kutokana na kujua ana fedha lakini anakuwa hana mapenzi naye. Hapo lazima atatafuta penzi la nje ili afurahishe nafsi yake, kwa hiyo watu hawa kutoka nje sishangai.
Pili:
Tabia ya kutoridhika na mpenzi mmoja, watu wa aina hii huwa hawajisikii kula kitu cha aina moja kwa muda mrefu, lazima atatafuta mtu wa kumfanya abadili mboga.
Vitu hivi vyote huwa vinawachanganya watu, hasa wale wanaoamini kuwa mwanaume anapokuwa na fedha au mwanamke anapokuwa mzuri, ni kila kitu katika mapenzi.
Mapenzi ni bahati, hasa kumpata uliyemkusudia, basi muombe Mungu utakayemchagua naye awe kweli amekukubali, hata ukiwa mbali kila mmoja amlindie mwenzake heshima, kwa kutanguliza uaminifu mbele.
Tukutane wiki ijayo.

Kuachana si uamuzi wa Pupa,inahitaji umakini, kujipanga




Pokea maneno yangu na uyasome kwa mtindo wa katikati ya mstari, mwisho utajua nini ambacho kinamaanishwa. Siwezi kushadadia utengano kwa maana najua athari na machungu yake.

Upo uhusiano ambao umelengwa kudumu, hasa kwa wanandoa.  Kuna wengine hawana sura ya kudumu, wapo kwa muda kwa kuzingatia mazingira pamoja na kile kilichomo ndani ya nafsi zao.

Unaweza kujiuliza; Kwa nini ufike wakati utake kuvunja uhusiano wako na mwenzako? Iwe wa kirafiki au kimapenzi, Ipo wazi kwamba kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuwafanya wahusika kuamua.

Yawezekana uhusiano wako na mpenzi au rafiki yako wa jinsia tofauti unakutia hasara, au unakuharibia biashara, au unakupunguzia heshima katika jamii, au pengine uaminifu wako kazini. 

Mathalan, mpenzi wako anafahamika kuwa ni kahaba. Inawezekana uhusiano wako na mwenzako unaidhuru nafsi yako. Mfano, mwenzio ana nguvu sana juu yako kiasi kwamba huwezi kusema “hapana” kwa lolote analokwambia. 

Pengine kutokana na hali hiyo umekuwa ukilazimika kufanya mambo ambayo huyapendi na ambayo hayaendani na maadili.

Lakini pia yawezekana umeanza kumchukia mwenzako.  Mazingira yamebadilika, kwa hiyo wewe na yeye hampatani tena. Unajitazama na kugundua kwamba ulivyo huendani naye. Ni matokeo ya kuchokana!

Uhusiano wowote unapoyumba, uwe wa kirafiki au kimapenzi, huwaweka wahusika katika wakati mgumu kiasi kwamba ni lazima mmoja achukue hatua ili aweze kuishi kwa amani na furaha ya kweli.

Hata hivyo, ikae akilini kwamba inauma mno kuachana na mtu unayempenda!
Kumaliza uhusiano wa kimapenzi au kirafiki si hatari, lakini la msingi ni kuhakikisha kuwa unamwacha mwenzako akiwa hajaathirika kisaikolojia kwa namna yoyote. 
Kwa sababu hiyo unapaswa kujifunza njia sahihi za kumaliza uhusiano wako na mwenzako inapobidi.

Kuna jamii inaweza kuthubutu kusema, unapochoshwa na mtu, mchukue uende naye mahali kisha umueleze kwa uwazi kuwa hutaki tena kujihusisha naye kwa sababu moja, mbili, tatu. 
Hata hivyo, hilo si jambo rahisi kwa wengi. Badala ya kukabiliana na mtu ana kwa ana na kumweleza kuwa humhitaji tena, zipo njia za kirafiki ambazo unaweza kuzitumia bila kusababisha matatizo yoyote ya kisaikolojia.

Friday, June 28, 2013

WHAT IS REAL LOVE?



Real love is something so deep, so energizing, that you will not know it unless you experience it. Love is an expression of energy, not something that is transacted. Tell me one thing: can you love people when you meet them for the first time? (From the audience: No Swamiji! We don’t even know them, then how can we love them?)


Exactly! This is what you think. Let me tell you, with a little bit of intellectual understanding andmeditation, you will realize that you can love anyone without a reason, causelessly! You can love the trees on the road, you can caress them and feel the energy flow from you. You can love people whom you pass by on the road without even knowing them. Love is actually your very being, not a distilled quality that you possess.

Nothing is as misconstrued as love is today. Today, love is more of a transaction. If someone says something nice to you, you love him; tomorrow if the same person falls short of it, you don’t love him that much or you probably hate him.

Even your lifelong friend, with whom you chat everyday on the computer, will seem suddenly not-so-close if he says something that goes against your approval. Where is your love at this time? It has suffered temporarily!

It is just games that you play; a game in which love and hate surface alternately and interchangeably. And this love-hate relationship is not love at all. Be very clear. It is simply your reaction to a person or a situation, that’s all. This is what we call love. This is not real love. It is subjective love, that’s all.

Real love knows no object. It is simply there whether there is an object or not. Real love is the subject itself. It does not know any object. You are the subject and you have become love, that’s all. Any object that comes in touch with it, feels it. Just like a river flows naturally and people enjoy it at the different places that they encounter it, real love exudes from a person and the people around him will be able to feel it.

There is absolutely no room for conditioning in real love. The energy in you should overflow and express itself as love. It is then that you can break through the highly knotted boundaries of relationships and express yourself beautifully, as a loving being!

In order to discover the quality of your being, that is love, two things can be done. The first thing: repeatedly listen to words like these so that they create a conviction in you about real love; so that a space is created in you for the process of transformation. Second thing: meditate so that the transformation can actually happen.

In practical life, when you go deeper and deeper into relationships, you will understand that all that you feel is not real love, but just some form of give and take. It is all just adjustment, some compromise, some duty-bound feelings, some fear, some guilt. It is all there in the name of love.

Meditation will take you beyond these mis-understandings of love. Meditation will work at the being level. That is why it is a shortcut! When you have to go through life and know it by yourself, it will take you a lifetime. But withmeditation, a space opens inside you to experience these things clearly for yourself, whatever your age may be.
Just understand this one thing: when you are able to love without a reason, you will expand like anything. Your world will suddenly seem larger than life. It will be so ecstatic. You will become an energy source to yourself and to others. You will be so overflowing that the energy in you has to touch others. There is no other way. Others will be naturally drawn to you.

Siri 20 usizozijua za kufurahia mapenzi..kutoka kwa"Joseph Shaluwa"


Mtazamo wako juu ya mapenzi utakuwa mwingine kabisa, huwezi kubabaishwa kamwe. Bila kupoteza muda, rafiki zangu, hebu twende tukaone siri zinazofuata.

3. MPE UHURU
Wengi wanaamini kumbana mpenzi ni njia sahihi ya kumfanya awe mwaminifu, si kweli. Kuna wenye tabia ya kuvizia simu za wenzao na kuzipekua, si utaratibu mzuri. Mpe uhuru, usimbane! Kuonesha kumwamini sana mpenzi wako, kunamfanya naye aishi ndani ya uaminifu.
Kumchunga hakumnyimi kuendelea na mambo yake, sana sana atafanya kwa siri kubwa. Kumpa uhuru, kutamwogopesha, atajua yupo na mwaminifu ndiyo maana hafuatiliwi, hapo utakuwa umechochea naye awe mwaminifu kama wewe.

4. ACHA PAPARA
Katika hatua za mwanzo kabisa za uhusiano wenu, hutakiwi kuwa na papara katika jambo lolote. Kila kitu kifanywe kwa utaratibu. Huna sababu ya kurukia mambo, hasa makubwa.
Wengi wamekuwa na haraka sana ya kukutana kimwili, haya ni makosa makubwa sana. Haraka ya nini kama unatarajia awe wako wa maisha. Ngoja nikuambie rafiki yangu, unapoanza kuulizia mapema mambo ya faragha, unamfanya mwenzako ashindwe kukuamini.
Kwanza, atahisi wewe upo kwa ajili ya kutaka kujistarehesha tu, lakini pia anaweza kufikiria kwamba unapenda sana mambo ya chumbani. Kumfanya agundue kasoro hiyo ni tatizo kubwa sana kwako.
Hata hapo baadaye mtakapoingia kwenye ndoa, ni rahisi zaidi kukumbuka mambo ya zamani, kwamba yupo na mtu anayependa sana mambo ya mahaba. Kwa maneno mengine, hata akihisi tu au kusikia kwamba una mtu mwingine pembeni, atapeleka moja kwa moja hisia zake kwenye kuamini moja kwa moja juu ya jambo hilo.
Papara si jambo jema kabisa kwa mwenzi ambaye unatarajia awe wako wa maisha. Tulia, mchunguze kwanza. Kumbuka unatakiwa kufikiria kuhusu mustakabali wa maisha yako ya baadaye, kama ndivyo, huna haja ya kuharakisha mambo ya mapenzi.

5. JENGA URAFIKI
Ukitaka kutengeneza uhusiano wenye nguvu, basi zingatia zaidi urafiki. Kumfanya mwezi wako rafiki ni silaha kubwa na yenye nguvu katika kuuimarisha uhusiano.
Mwenzi wako anapojiona kama rafiki, anakuwa katika nafasi nzuri ya kuzungumza chochote, ikiwemo matatizo na migongano mbalimbali kama rafiki zaidi.
Hawezi kukuficha siri zake. Atakuwa na wewe muda wote na atakusogeza karibu yake kwa kila kitu. Hata penzi lenu pia litakuwa na nguvu zaidi. Urafiki ni kila kitu ndugu zangu.
Acha tabia ya kumkaripia mpenzi wako, jenga mazoea ya kujadiliana zaidi kuliko kutumia kauli za ukali. Rafiki zangu, yote hayo niliyoyazungumza yanajengwa na jambo moja tu; urafiki!

6. MSIFIE
Wengine wanaweza kushangazwa na kauli hiyo, lakini nataka kuwaambia kuwa kati ya mambo muhimu kabisa kumfanyia mpenzi wako na kulifanya penzi kuwa jipya ni kumsifia. Unapomwambia mwenzako kauli nzuri za kumbembeleza kuwa yeye ni mzuri, anakuvutia kwa kila hali, unajenga penzi.
Unamfanya anajihisi wa thamani, atajiamini kuwa yeye ni mkamilifu, si kwa watu wanaomzunguka pekee, bali hata wewe ambaye umemchagua na kumfanya awe wako.
Kama huna utamaduni wa kumsifia mpenzi wako, huu ni wakati wako wa kufanya hivyo kwa lengo la kuzidisha mapenzi na kuyapa nguvu.

7.  SAIDIA KUKUZA UHUSIANO WENU
Kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha penzi linazidi kukua siku hadi siku. Kwa maana hiyo, wewe kwa nafasi yako unatakiwa kuhakikisha unakuwa mstari wa mbele kukuza uhusiano wenu.
Kuna mambo mengi sana ambayo yakifanyika, yanakuza uhusiano. Vipo vitu vya kufanya, kutoka pamoja ni njia mojawapo ya kukuza uhusiano. Rafiki zangu, mnapokwenda katika matembezi, husaidia kubadilisha mapenzi na kuonekana mapya.
Si lazima kwenda nje ya mji, kikubwa ni kuzingatia mfuko wako. Hata mkienda mahali pa kawaida tu, mkanywa juice na keki, bado ni nafasi nzuri kwenu ya kukuza uhusiano huo.
Kila mmoja ana wajibu wa kufanya hivyo, lakini hutakiwi kumsubiri mwenzako afanye, wewe kwa nafasi yako unatakiwa kuhakikisha unamfanya mwenzi wako afurahie uhusiano wenu. Kufanya hivyo, kutampa deni na yeye la kufanya hivyo kwako.
Bado kuna siri nyingi zimesalia, wiki ijayo tutaendelea. Tukimaliza kumi za kwanza, tutaingia kwenye siri nyingine kumi za mwisho ambazo zitakuwa zinahusu mambo ya ndani zaidi ya ndoa.

Msingi imara ndiyo tiba ya matatizo yenu.


NAAM tumekutana tena kwenye kona hii ya mahaba. Kama kawaida ndani ya uhusiano kuna maudhi yaliyofikia hatua ya kukosa uelewano ndani.
Nitakuwa si muungwana kwa kutotanguliza salamu, mimi ni mzima wa afya njema, sijui wewe mwenzangu?
Nimepata maswali mengi juu ya matatizo ndani ya ndoa au uhusiano.

Ni matatizo gani hayo?
Kukosekana amani ndani ya nyumba zetu, heshima na upendo kutoweka huku ikiwa haijulikani nani baba, nani mama wote mmekuwa kambale kina mmoja ana sharubu.

Katika swali la msingi la ndugu yangu linatokana na tabia za mkewe kujiamulia mambo bila woga kama anajimiliki mwenyewe.
Yupo na mkewe muda mrefu sasa na wana watoto wawili ambao ni wadogo, ila kama isingekuwa hivyo angekuwa ameishamuacha muda mrefu. Kikubwa alikuwa akiomba msaada wa ushauri ili aepukane na dhahama za mkewe.

Nina imani wote swali mmelisoma, naamini ukipewa nafasi ya kushauri ungeanzia kwenye tatizo. Lakini kwangu mimi huwa sijibu tatizo bali chanzo cha tatizo ili mwingine yasimkute kama yaliyomkuta mwenzetu.
Hebu sasa tuangalie tatizo hilo linatokana na nini?
Kama nilivyoanza na kichwa cha habari kuwa msingi imara ndiyo tiba sahihi ya matatizo yenu.

Ni msingi gani?
Nina imani ni swali lililo akilini mwako.
Siku zote nyumba iliyo bora, ni ile yenye msingi imara ambao ndiyo unaobeba nyumba nzima atakayodumu daima dawamu.
Hata katika kitu chochote kama mapenzi au biashara msingi imara ndiyo unaoendesha kitu imara. Leo nazungumzia uhusiano wetu ndani ya nyumba kati ya mke na mume.

Hili ni tatizo linalotafuna uhusiano wetu:
Kuna tatizo moja ambalo huenda watu huwa hatulioni mwanzo tunapoanzisha uhusiano wetu, tatizo hili ni udhaifu wa mtu kushindwa kuwa kiongozi wa nyumba kutokana na baadhi ya vitu akiamini akivikemea huenda akaharibu uhusiano wao.

Mara nyingi mwanzo wa mapenzi wanaume wengi huwa dhaifu kwa wake zao kutokana na uchanga wa ndoa zao, huku wakitaka kuonyesha mapenzi kwa wenza wao. Hata linapotokea jambo la kuudhi au kwenda kinyume hawawakanyi, bali hulikemea kwa kubembeleza huku ikionesha wazi mtendaji anaweza kuamua mwenyewe iwe kuendelea kutenda au kuacha.

Unapoyafumbia macho makosa madogo madogo na kuamini ipo siku utayakataza, ni sawa na kuuacha ufa uliouona kwenye nyumba yako, jinsi unavyouacha ndivyo unavyokua.

Ukija kushtuka na kuanza kulikemea kwa nguvu, hapo lazima mwenzako ataona unamuonea kwa vile kitu kile alikuwa akikifanya kwa muda mrefu pengine miaka sita iliyopita, ulikuwa ukitazama tu na yeye kujiona yupo sawa japo akili yake inamsuta kwenda kinyume.

Hapa ndipo tunapata jibu la ndugu yetu kuwa ugonjwa aliuacha kipindi kirefu mpaka umekomaa. La muhimu ni kujenga msingi imara toka mwanzo wa uhusiano kwa kukemea yote kwa nguvu zote bila kuangalia umbile wala sura.

Kama mkeo ana tabia hizo bado hujachelewa, mweke chini na kukemea mabo yote anayotenda kinyume. Kama hataki kusikia, ni wazi si mwenzako katika safari ya maisha, uamuzi unao mwenyewe kuangalia kama kuwa naye ni faida au hasara kwako. Kama ni faida endelea naye kama ni hasara jibu unalo mwenyewe.

Mwanamke aliyetoka katika familia inayojua ndoa ni nini, ni msikivu kwa kila atakachoelezwa na mwenzake kwa faida ya ndoa yake. Ni mwenye tabia za kike za upole na usikivu, kumuheshimu mumewe na kuacha asichokipenda.

Hakuna sifa ya kushindana kila kitu na mumeo kwa kupaza sauti, mwanamke mwenye silika la kike huwa hapazi sauti juu, ni mwenye aibu.

Usisubiri mpaka afikirie kutafuta wa kumtuliza!


NILIWAHI kuandika kabla, leo narudia tena, jinsi unavyoishi leo ni matokeo ya ulivyokuwa ukiishi zamani. Kama unaishi maisha magumu na tabu zinakuandama kila kona, vuta picha uangalie miaka mitano nyuma ulivyokuwa ukiishi.
Rafiki zangu, pointi kubwa hapa ni kwamba, unatakiwa kuangalia kila hatua ya maisha yako ya sasa kwa maana ni mtaji wa jinsi utakavyoishi siku zijazo. Ukiwa mtu wa kuwaombea wenzako mabaya, kuwasengenya, kuwasimanga, kuwadharau, kukatisha tamaa n.k, majibu yake utayapata baadaye!
Ukimchukia binadamu mwenzako leo kwa sababu ana vitu ambavyo huvipendi au sababu zako binafsi ni wazi tayari mtakuwa mnatengeneza uadui. Kama ndivyo, kesho anaweza kukusaidia? Jaribu kuvuta picha, unakorofishana na watu wawili kila mwezi, maana yake kwa mwaka utakuwa na watu 24 ambao hamzungumzi! Hebu zidisha mara miaka mitano. Utaishije?
T
ukiachana na hilo, hebu twende katika mfano mdogo sana wa kawaida; Utakuta mtu leo hii anatumia fedha zake hovyo kwa kulewa na anasa nyingine zisizo na maana, haweki akiba na mipango ya matumizi ya fedha, miaka kumi ijayo atakuwa wapi? Bila shaka atakuwa akipata shida analalamika na kuanza kukumbuka maisha yake yaliyopita. Utamsikia: “Niliwahi kufanya kazi wizarani, nilikuwa na nafasi nzuri sana....yule nanii tulisoma naye...”
Itakusaidia nini? Kujisifu kuwa mtu fulani maarufu ulisoma naye au ulifanya naye kazi katika kitengo fulani nyeti itasaidia nini? Angalia umesimamia wapi? Rafiki zangu, kama ukisoma maneno haya kwa maana ya kupima na kuyafanyia kazi, huwezi kujuta siku zijazo za maisha yako. Msingi mzuri wa kesho, huanza kujengwa leo.

Hii ipo hata katika mapenzi, unakorofishana na mpenzi wako leo, mnagombana na kuachana. Kesho akienda kuoa au kuolewa na mwingine, unaanza kujilaumu. Haitakusaidia kitu ndugu yangu. Jipange na ufanye kila kitu katika maisha yako huku ukiangalia mustakabali wako wa kesho.
Unapokuwa kwenye ndoa, lazima ujue kusoma alama za nyakati. Kuna wakati mambo yanaweza kubadilika ndani ya nyumba, lakini kuna taratibu fulani ukianza kuona kama zinataka kujirudia ujue kabisa kuna kitu kinatakiwa. Nazungumzia suala la tendo la ndoa. Wapo watu walioumbwa tofauti.
Wengine wanaweza kusema wazi kabisa: “Leo mama nanii nataka,” mwingine akasema: “Dear leo nina hamu sana na wewe,” lakini wapo ambao hawawezi kusema chochote! Vitendo vinaongea...
Hawa ndiyo ninaowazungumzia leo. Rafiki zangu, ukiwa na mwenzi wa aina hii na usipokuwa makini kujua kuwa mwenzako anakuhitaji ni rahisi kumuacha na kiu yake, lakini wakati huo ukawa unamwachia mlango wa kutafuta mwingine ambaye anaamini ataweza kutuliza maruhani yake kwa wakati.
Wenye tatizo hili hasa ni wanawake; Wanaume wengi si waoga kusema wanawahitaji wenzi wao faragha. Tena wao ndiyo huwa waanzilishi wa kila kitu. Anaweza kutoka kazini akiwa hana wazo kabisa na jambo hilo, lakini akifika nyumbani ghafla anajisikia kukutana na mwenzake.
Hafikirii mara mbili, ataanza visa na michezo midogomidogo, mwishowe kazi inakamilishwa. Ndivyo walivyo. 

Kazi ipo kwa wanawake ambao sasa wapo katika makundi matatu; Machakaramu wanaoweza kusema moja kwa moja WANATAKA, wanaozungumza kwa vitendo na wale wakimya wanaosikilizia amri kutoka mwanaume.
Makundi yote haya yanahitaji umakini mkubwa. Athari kubwa ni kwamba ni rahisi kusalitiwa kama hutakuwa makini katika kuchunguza alama za nyakati na uhitaji wa mwanamke wako. Rafiki zangu, ndoa ni kitu ghali kuliko kingine chochote duniani.
Ni agano ambalo linatakiwa kuheshimiwa, kulindwa na kupewa kipaumbele. Hata kama una kazi nzuri, ikiwa nyumbani kwako kuna tatizo, cheo chako si chochote. Kama mke wako analalamika humfurahishi kiasi kwamba anaanza kufikiria kutafuta mtu mwingine nje ni tatizo.
Nimeanza na dodoso rafiki zangu, wiki ijayo tutaingia kwenye mada yenyewe ambapo tutaangalia kwa kina makundi hayo na tabia zake.
Kidogo ina mambo yake lakini nitajitahidi kuzungumza kwa lugha ya kirafiki zaidi ili ujumbe ufike vyema bila kuharibu hali ya hewa.
                                             Mada na  Joseph Shaluwa